MAONESHO ya uwekezaji na viwanda katika Mkoa wa Ruvuma yamefanyika kuanzia Julai 24 hadi 26 katika uwanja wa Majimaji mjini Songea.Maonesho hayo yamefunguliwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa.Katika uwanja huo kulikuwa na vibanda vya maonesho zaidi ya 50.Hata hivyo banda la Manispaa ya Songea lilikuwa ni miongoni mwa mabanda ambayo yalivutia wengi hasa kutokana na kuonesha vivutio vya utalii katika Manispaa ya Songea na maeneo ambayo yanafaa kwa uwekezaji katika Manispaa hiyo likiwemo eneo maalum la Mwengemshindo ambalo lina eneo lenye ukubwa wa hekari 5000.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa