HATIMAYE Kampuni ya kimataifa ya China inayoitwa China Sichuan International Co-operation ndiyo imeshinda tuzo ya Zabuni ya kuendelea na ujenzi wa barabara za Manispaa ya Songea kwa kiwango cha lami nzito.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akizungumza na wafanyabiashara wa Manispaa ya Songea kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea amesema Kampuni hiyo inatarajia kuanza kazi Machi 23 mwaka huu ambapo utajenga barabara zenye urefu wa kilometa 10.3.
Hata hivyo Mndeme amemuomba Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea kufanya marekebisho ya muda katika eneo la Majengo mwezi huu wakati Mkandarasi anasubiriwa kuanza kazi mwezi ujao.
Halmashauri ya Manispaa ya Songea ilivunja Mkataba wa ujenzi wa lami nzito yenye urefu wa kilometa 8.6 kati yake na Kampuni ya Lukolo yenye makao makuu yake Jijini Dar es salaam,baada ya Kampuni hiyo kukiuka mkataba.
Imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa