Baraza la madiwani Manispaa ya Songea limewasimamisha kazi watumishi wawili kutoka idara ya Afya na Idara ya Utawala kutokana na uzembe kazini.
Tamko hilo limetolewa tarehe 20 Novemba 2023 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea iliyohudhuriwa na Waheshimiwa madiwani, Wataalamu, viongozi wa vyama vya siasa, pamoja na wananchi mbalimbali ikiwa ni kikao cha robo ya kwanza kwa mwaka 2023/2024.
Awali kabla ya tamko hilo baraza la madiwani lilianza kwa kutoa kiapo kwa diwani mteule Christopher Kayombo ambaye alishinda uchaguzi wa Udiwani uliofanyika kwa lengo la kuziba nafasi ya aliyekuwa diwani wa kata Marehemu Ajira Kalinga ambaye alifariki mwezi mei 2023.
Akizungumza Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Mhe. Michael Mbano alisema kwa mwaka 2023/2024 Manispaa ya Songea imepokea kiasi cha shilingi Bil. 4 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo imeanza kutekelezwa. “Alibainisha”
Amewataka wataalamu wote kuhakikisha wanasimamia miradi kwa ubora na kuhakikisha wanakamilisha mapema iwezekanavyo.
IMEANDALIWA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa