Baraza la Madiwani Manispaa ya Songea limepitisha bajeti ya shilingi 55,686,483.00 kutoka kwenye vyanzo mbalimbali katika kipindi cha mwaka wa fedha 2025/2026.
Baraza hilo limefanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea tarehe 12 februari 2025 ambalo lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali ngazi ya Chama, Waheshimiwa madiwani pamoja na wakuu wa idara na vitengo na wadau mbalimbali kwa lengo la kupitisha rasimu ya mpango na bajeti ya mwaka 2025/2026.
Akisoma taarifa hiyo kwenye baraza la Madiwani Mchumi wa Manispaa ya Songea Wilfredy Razaro alisema, vyanzo vya mapato ni kiasi cha sh. 8,318,668,000.000, mishahara ni shilingi 36,990,880,000.00, matumizi mengine kutoka Serikali kuu shilingi 1,874,749,000.000 ambapo ruzuku ya miradi mbalimbali ya maendeleo ni 3,563,995,000.00 na vyanzo vya ndani Halmashauri hiyo ni 4,938,619,483,000.
Razaro alibainisha vipaumbele katika Halmashauri hiyo ni kutoa nafasi kwa watumishi kujiendeleza kupitia semina, mafunzo ya muda mfupi na mrefu kwenye vyuo mbalimbali pamoja na semina na mikutano ya kitaaluma, kutenga madeni ya watumishi na zabuni, upatikanaji wa vitendea kazi, stahiki mbalimbali za watumishi, Mazishi, likizo pamoja na matibabu. “Alieleza”
Aliongeza kuwa vipaumbele vingine ni ununuzi wa gari kwaajili ya kurahisisha utendaji wa kazi wa watumishi katika kusimamia majukumu pamoja na mahitaji maalum kutokana na wagonjwa kwa ustawi wao kazini.
Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano kwa kushirikiana na Madiwani hao mara baada ya kuridhia na kupitisha rasimu ya mpango na bajeti 2025/2026 amewataka madiwani hao kuendelea kutoa ushirikiano katika kusimamia miradi ya maendeleo inapoelekea kipindi cha uchaguzi huku akiwataka kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo.
Akitoa pongezi kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo maji, elimu, barabara na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi.
Kwa upande wakeMbunge wa jimbo la Songea Mjini Dkt. Damas Ndumbaro (MB) Waziri wa Katiba na Sheria amewataka madiwani kujipongeza kwasababu ya kuteuliwa kwa Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza wa nafasi ya makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa ambapo kupitia mkutano mkuu wa CCM Taifa ulimpendekeza Dkt. Samia Suluhu Hassani kuwa mgombea wa Urais na Dkt. Hussein Mwinyi kuwa mgombea Urais Zanzibar.
Dkt. Ndumbaro alisema kila kata kuna miradi ambayo imetekelezwa hivyoMadiwani mna haki ya kujivunia kutokana na utendaji wa kazi zilizofanyika.
MWISHO:
NA AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa