Baraza la Madiwani Manispaa ya Songea limeidhinisha makisio ya bajeti ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kiasi cha Tsh 39,046,546,758.33 kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya Halmashauri.
Mstahiki Meya Halmashauri ya Manispaa ya Songea Michael Mbano ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la Madiwani alisema kwa kupitia baraza hili tumeidhinisha mpango na bajeti ya maendeleo wa mwaka wa fedha 2021 hadi 2022, hivyo ametoa rai kwa madiwani hao kutoa ushirikiano kwa wataalamu katika kusimamia miradi ya maendeleo iliyopo kwenye maeneo yao.
Baraza hilo limefanyika tarehe 01 machi 2021 na kuidhinishwa kukusanya na kutumia kiasi cha fedha 39,046,546,758.33 kwa ajili ya miradi mabalimbali ikiwemo na miradi ya maendeleo. Kati ya fedha hizo mapato ya ndani ni kiasi cha Tsh cha shilingi 4,329,012,060.00 makisio ya mapato ya ndani ambayo ni Zaidi ya shilingi 354,757,770.00 sawa na asilimia 8.2 ukilinganisha na makisio ya mwaka 2020/2021 yalikuwa 3,974,254,060.00.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Tina Sekambo alisema katika mpango na bajeti ya maendeleo wa mwaka wa fedha 2021/2022, Halmashauri ya Manispaa ya Songea inatarajia kukusanya na kutumia kiasi cha shilingi 6,793,556,522.33 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo na mapato halisi ya ndani, ruzuku ya Serikali kuu, na Wahisani.
Tina alisema kuwa fedha hizo zitazokusanywa kutoka kwenye mapato mbalimbali ndizo zinazokwenda kutekeleza miradi ya maendeleo. Hata hivyo, Amewataka madaiwani hao kutoa ushirikano kwa wataalamu wakati wa kutekelezaji wa zoezi la ukusanyaji wa mapato ili kuweza kufanikisha kutatua changamoto mbalimbali zinzoikabili Halmashauri hiyo.
Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya Hamisi Abdalah Ally akichangia hoja katika baraza hilo ambapo amewataka Madiwani hao kuitisha mikutano ya wananchi kwenye kata zao na kuwashirikisha wataalamu kwaajili ya kusikiliza kero na malalamiko na kuzitafutia ufumbuzi haraka iwezekanavyo badala ya kusubili viongozi wa ngazi ya juu kuja kutatua kero zao.
Hamisi aliongeza kuwa wananchi wana kero nyingi na ninyi Madiwani ndiyo wawakilishi kupitia maeneo yenu lakini hamuitishi mikutano. Endapo mtawashirikisha wataalamu kwenye mikutano hiyo mtaondoa kero zinazowakabili wananchi kwani wataalamu na Madiwani ni ndugu hufanya kazi kwa kutegemeana.
Naye Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Dr. Damas Ndumbaro ambaye ni Waziri wa Maliasili na Utalii alisema kila Wilaya ilipangiwa kuwepo kwa hospitali ya Wilaya lakini baadhi ya Wilaya ina Halmashauri Zaidi ya moja, hivyo kutokana na changamoto hiyo Serikali imeweka mpango wa kujenga Hosptali kila Halmashauri lakini haizuwii kuweka mkakati wa ujenzi wa Hosptali ya Mkoa .
Dr. Ndumbaro (MB) alimpongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea pamoja na Wataalamu wate walioshiriki kuandaa mpango na bajeti hiyo ambayo imezingatia vitu muhimu.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
02.03.2021
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa