BARAZA la Madiwani la Manispaa ya Songea limetoa maamuzi kwa watumishi wanne wa Halmashauri ambao walikuwa wamesimamishwa kazi.Akitangaza maamuzi hayo kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea Mwenyekiti na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Alhaj Abdul Hassan Mshaweji amemtaja mtumishi mmoja kati ya wanne uchunguzi umebaini kuwa hana makosa hivyo yuko huru kuendelea na kazi ambapo amemtaja mtumishi huyo kuwa ni Mkaguzi wa Ndani Joel Mantakara.
Mshaweji awataja watumishi watatu wamekutwa na hatia akiwemo Afisa Mapato Juliana Rocky amekutwa na makosa nane hivyo Baraza limeamua afukuzwe kazi na kwamba Mweka hazina Denis Mwaitete na Afisa Mapato Salum Mwandu,Baraza limeamua wapunguziwe mshahara katika kipindi cha mwaka mmoja.Mshaweji amesisitiza watumishi kufanyakazi kwa uaminifu mkubwa kwa masilahi ya umma na wananchi wa Manispaa ya Songea.
"Baraza linatoa onyo kwa watendaji kufanyakazi kwa uaminifu,hatutasita kutoa adhabu kali zaidi kwa mtumishi yeyote ambaye atabainika kutafutana fedha za umma''.alisisitiza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea na kuongeza kuwa Baraza la madiwani limejipanga kuhakikisha kuwa mapato ya manispaa yanaongezeka hadi kufikia asilimia 100 na kwamba upotefu wa fedha kiasi cha shilingi milioni 118 umesababisha hasara ya asilimia 4.4 ya mapato katika Manispaa hiyo.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa