BARAZA la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC) kwa kushirikiana na ofisi ya Waziri Mkuu chini wakufunzi wake wametembelea wajasiriamali mbalimbali ambao wamajiajiri katika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Wajasiriamali ambao wametembelewa ni wale ambao wamepata mafunzo yanayotolewa na Baraza la taifa la uwezeshaji na wakatoa ushuhuda wa jitihada zao ambazo wamezifanya na kupiga hatua katika miradi yao ambayo imewasaidia kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wake, Mwanakikundi wa Kona To Kona Nasma Abubakary akizungumza ofisini kwake ameelezea jinsi walivyoshirikiana katika kuanzisha kikundi chao ambacho kinajishughulisha na kutengeneza bidhaa za ngozi kama vile mikanda ya ngozi, viatu vya ngozi (sendo), eleni, bangili, Mapazia ya mianzi na mikufu. Ambapo kupitia mradi huo umetemgeneza ajira kwa vijana wanne ambao wote wanafaidika.
Abubakary amesema kuwa pamoja na mafanikio yote ambayo wamefanikiwa kuyapata tangu wameanza mradi pia ameeleza kuwa kuna changamoto ambazo zinawakwamisha kama vile mashine na mitaji na ameweka wazi kuwa kutokana na mafunzo ambayo wameyapata yatawasaidia katika kuzikabili changamoto mbalimbali ambazo zilikuwa zinawakwamisha katika kufikia malengo yao.
“Elimu tuliyoipata inatosha na itatufikisha pale tulipolenga.”
Naye, Mjasiriamali Selemani Faraji Twaibu ambaye ni mwanakikundi wa Matogoro Stick Industry ameeleza umuhimu wa vijana kujiajiri na ametoa shukrani kwa Baraza la Taifa la Uwezeshaji kwa kuwapa mafunzo ambayo yatawawesha kupiga hatua zaidi katika biashara zao.
Pia Twaibu ameeleza kuwa ili waweze kufanikiwa zaidi ameiomba serikali kuendelea kuwaunga mkono kwa kuboresha mikopo ambayo itawasaidia kupata mitaji ambayo watahitumia katika kukuza na kuboresha huduma zao.
Baraza la Taifa la Uwekezeshaji lipo katika Mkoa wa Ruvuma kutoa elimu ya ujasirimali na biashara kwa vijana wenye umri kati ya miaka 18 hadi 35 ambapo zaidi ya vijana 150 wamenufaika na elimu hiyo..
Imeandaliwa na
Bacilius Kumburu
Wa kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Songea
Agosti 14, 2019.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa