Kwa mujibu wa sheria kifungu cha 13 cha sheria ya Marekebisho ya mwaka 2021 Namba 3 Baraza la kata lina haki ya kufanya Suluhisho na si kutoa Hukumu.
Baraza la ardhi ya Kata hayana Mamlaka ya kufanya Suluhisho bali ameyataka Mabaraza hayo kuendelea kufanya usuluhisho wa wa kimahakama ili kuondoa migogoro mbalimbali.
Hayo yametamkwa kwenye Baraza la Madiwani la Mwaka la Hesabu za Serikali 2023/2024 lililofanyika leo tarehe 30 Agosti 2024 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea ambalo lilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali ngazi ya Wilaya, Vyama vya Siasa, Wataalamu, pamoja na Wananchi kwa lengo la kutoa taarifa ya kufunga hesabu za Serikali za mwaka.
Akizungumza Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Mheshimiwa Michael Mbano amezitaka Idara na Vitengo vyote vyenye hoja za ukaguzi zisizo jibiwa wahakikishe wanajibu hoja zote kabla au ifikapo tarehe 30 Septemba 2024.
Mhe. Mbano amewataka wataalamu hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa Wakaguzi wa hao ili waweze kumaliza kujibu hoja zao kwa kutoa majibu sahihi na kukamilisha kwa wakati.
Kwa Upande wake kaimu Mweka hazina Manispaa ya Songea Mustafa Matili alisema Hesabu za Halmashauri zilifungwa kulingana na agizo namba 31 kifungu kidogo cha 1 hadi cha 6 cha muongozo wa fedha za Serikali za Mitaa za Mwaka wa fedha 2009 kwa kuzingatia sheria za fedha za Serikali za Mitaa kwa kufuata kanunni ya ufungaji wa hesabu za Serikali za Mitaa kimataifa namba 1 hadi 34. “Alibainisha”
Naye Katibu Tawala Wilaya ya Songea Mtella Mwampamba amesema Nanukuu” Mabaraza ya Ardhi /Ndoa hayatakiwi kutoa hukumu au taraka bali yanatakiwa kufanya suluhisho kwasababu suala la ndoa hukumu yake inagusa haki ya mtu hivyo ameyataka mabaraza ya kimila, na mabaraza ya ndoa kutoa Suluhisho. Mwisho wa Kunukuu.
Akitoa salaamu za chama cha Mapinduzi Mkutanoni hapo, Katibu wa CCM Songea Mjini Komredi James Mgego amesema, kuanzia tarehe 02 hadi 04 Septemba 2024 kutakuwa na ziara ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma ambapo atatembelea miradi katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea kisha atahitimisha kwa kuzungumza na viongozi wa dini, na Wazee.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa