MAMLAKA ya Udhibiti wa Chakula na Dawa ( TFDA ) katika Manispaa ya Songea imekamata diapers( Nepi) ambazo muda wake umemalizika tangu Agosti mwaka huu zikiendelea kuuzwa katika moja ya maduka yaliopo soko kuu la songea.
Mratibu wa TFDA katika Manispaa ya Songea Vitalis Mkomela àmesema TFDA imekamata nepi aina ya ponpon 65 zenye thamani ya shilingi 277,500 ambapo mmiliki amekiri kuuza bidhaa ambazo muda wake umemalizika hivyo amepigwa faini ya shilingi zaidi ya lakini moja ikiwemo gharama za kuteketeza mzigo huo.
Mkomela anaèndelea kutoa raia kwa wananchi kabla ya kununua bidhaa kusoma maelezo yanayoonesha bidhaa ilitengenezwa lini na mwisho wa muda wake wa matumizi (Expired date ).
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa