Taasis ya kuzuia na kupamba na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma imefuatilia zaidi ya Bil. 10.6 fedha za miradi ya maendeleo iliyopo katika Halmashauri mbalimbali Mkoani Ruvuma.
Hayo, yamejiri katika kikao cha Waandishi wa Habari kilichofanyika katika ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma kwa lengo la kutoa taarifa ya utekelezaji wa ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo katika kipindi cha robo ya januari hadi Machi 2024.
Akizungumza Bi Janeth Haule Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma alisema “ ufuatiliaji huo umefanyika katika miradi ya ujenzi wa madarasa na vyoo katika shule ya Sekondari, ujenzi wa bweninna ukarabati wa chumba cha maabara zilizoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Namtumbo, Madaba, Nyasa, na Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kwa thamani ya shilingi 3,449,954,835.60.”
Miradi mingine ni pamoja na ujenzi wa nyumba za watumishi ikiwemo na nyumba ya Mkurugenzi na wakuu wa idara katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, ujenzi wa nyumba ya walimu 2 moja katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, Tunduru,zenye thamani ya mil. 838,859,638.
Aidha ametoa wito kwa wananchi Mkoani Ruvuma kuendelea kuunga mkono jitihada za kufichua vitendo vya Rushwa na wala Rushwa kwa kutoa taarifa sahihi zitakazowezesha kuwachukulia hatua wahusika hasa katika kipindi cha uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao unatarajia kufanyika mwaka huu.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa