Katika kutatua changamoto za Maji Mjini Songea, Serikali imesaini Mkataba kati ya Kampuni ya China Civil engeneering Construction Coorporation wa Shilingi Bilion 145.77 ambao umesainiwa tarehe 10 Machi 2023 ambao utatekelezwa kwa muda wa miezi 32.
Tukio hilo limefanyika chini ya usimamizi wa Naibu Waziri wa Maji Marypriska Mahundi ambaye alimwakilisha Waziri wa Maji lililofanyika Manispaa ya Songea kwa lengo la kusaini Mkataba wa kazi ya usambazaji wa maji ambao ni miongoi mwa miji 28 itakayonufaika na miradi huo.
Mhe. Marypriska amesema katika kuhakikisha jamii inapata maji safi na salama hawanabudi kutunza Mazingira katika vyanzo vya maji
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal. Laban Thomas amesema mradi huo utawezesha kuongeza uwezo wa kuzalisha maji kutoka lita Mil. 11.58 kwa siku hadi Mil 42.58 kwa siku ambao utaondoa kero ya maji kwa wakazi wa Songea.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa SOUWASA Eng Patrick Kibassa amesema Mamlaka ya Maji SOUWASA ina jumla ya vyanzao 13 vyenye uwezo wa kuzalisha maji Lita Mil. 11.58 kwa siku sawa na asilimia 57% dhidi ya mahitaji Mil 20.34 kwa siku.
Eng. Kibassa ameongeza kuwa huduma ya maji safi inapatika kwa saa 22 kwa siku ambapo Mamlaka inakabiliwa na changamoto ya kuzalisha maji lita mil.11.58 kwa siku dhidi ya mahitaji lita mil. 20.33 kwa siku a ambapo mahitaji makubwa ni ya Nishati ya Umeme ambayo Mamlaka inatumia Nishati Mil. 32 kwa mwezi ili kusukuma maji kwenda kwa wateja.
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa