Baraza la Madiwani Manispaa ya Songea likiongozwa na Mstahiki Meya Michael Mbano kwa kushirikiana na wataalamu wametoa Pongezi za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mhe. Samia Suluhu Hassani kwa kutoa kiasi cha fedha Bilion 1.520,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 76 katika shule za Sekondari.
Pongezi hizo zimetolewa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani liliofanyika tarehe 10 Oktoba kwa ajili ya kutoa taarifa za mapokezi ya fedha Bil. 1.52, na kupokea mrejesho wa mpango na bajeti ya Halmashauri iliyoidhinishwa na Serikali ambayo itatekelezwa mwaka wa fedha 2022/2023, pamoja na kupitisha majina ya wajumbe wa bodi ya maji kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea na kuhudhuriwa na waheshimiwa madiwani, wataalamu na wananchi.
Mhe. Mbano akielezea kuhusu mpango kazi na mikakati iliyojiwekea Manispaaa ya Songea katika kufanikisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 76 ni pamoja na kushirikisha wananchi kuhusu mapokezi ya fedha za mradi kwa kufanya mikutano ya hadhara ifikapo tarehe 11/10/2022 kwa kata zote na mitaa, pamoja na kufuata muongozo wa utekelezaji wa miradi hiyo.
Amewataka Madiwani na wataalamu kutumia nafasi zao kuwaeleza wananchi shughuli mbalimbali na mafanikio yanayotekelezwa na Serikali ili wananchi waweze kufahamu miradi ya maendeleo inayoendelea kufanyika katika Serikali yao.
Alisema miongoni mwa miradi inayoendelea kujengwa Manispaa ya Songea ni pamoja na kituo cha afya Lilambo kwa fedha za mapato ya ndani pamoja na vituo vya afya Mletele, kituo cha afya Subira, Kituo cha afya Msamala, Hospital ya Rufaa inyojengwa Mwenge mshindo, pamoja na Hpsptali ya Wilaya Songea kwa fedha kutoka Serikali kuu. “ Alibainisha”
Mh. Mbano amewaagiza maafisa watendaji wa kata na mitaa wote kuhakikisha wanaweka ulinzi shirikishi katika maeneo wanayoyaongoza ili kuzuwia matukio mbalimbali ya wizi wa ng’ombe ambayo yamekuwa tishio katika jamii na utekelezaji wa agizo hilo unatakiwa kuwasilishwa kwenye kikao kazi cha Madiwani ambacho kinatarajia kufanyika hivi karibuni. Alisisitiza
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Songea Andambike Kyomo alisema Manispaa ya Songea imepokea fedha kutoka Serikali kuu kiasi cha Bil.1.52 kwajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 76 ambayo yatajengwa katika mfumo wa FORCE ACCOUNT ambao unatakiwa kukamilika ifikapo tarehe 15 disemba ambapo utajumuisha utengenezaji wa samani ambazo ni viti 50 na meza 50.
.
Kyomo, akitoa maelekezo juu ya mrejesho na bajeti iliyoidhinishwa ambapo alibainisha kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa mwaka wa fedha 2022/2023 imeidhinishwa kukusanya na kutumia kutoka kwenye vyanzo mbalimbali jumla ya shilingi 45,635,750,000 kati ya fedha hizo, fedha za mapato ndani ni 5,517,867,000.00, shilingi 35,842,547,000.00 ni fedha za Serikali ambapo shilingi 4,275,336,000.00 ni fedha za wafadhili.
Akifafanua kuhusu namna ya uundaji wa Bodi ya maji Manispaa ya Songea “ kwa Mujibu wa Sheria namba 5 ya Maji na Usafi wa Mazingira 2019 ambayo inasema mchakato wa kuwapata wajumbe wa bodi ya maji ambao unapitia baraza la madiwani watapendekeza majina ya wajumbe watakaounda bodi mpya ya maji baada ya bodi iliyopita kumaliza muda wake na majina hayo yapitishwe kwenye baraza la madiwani ili yaweze kupelekwa Wizarani kwa ajili ya kuteuliwa kupitia nafasi za mjumbe mwakilishi wa watumiaji wa maji, mwakilishi wa wanawake, na mwakilishi wa madiwani. Mwisho wa kunukuu”
Mwanasheria kutoka SOWASA Abel Ngilangwa alisema kwa mujibu wa sheria na taratibu za kupata wajumbe wa bodi zinapitia katika mchakato wa kupata mjumbe mmoja kutoka Wizara ya maji, Mjumbe kutoka Mkoa na Halmashauri, mjumbe kutoka baraza madiwani, mjumbe kutoka kwa watumiaji wa maji, na mjumbe mwakilishi wa wanawake.
Ngilangwa alibainisha kuwa bodi ya maji Safi na Mazingira na mamlaka nyingine zinaongozwa kwa mujibu wa sheria namba 5 ya mwaka 2019 na kanuni zake za mwaka 2019 ambazo zinafafanua sifa za watakaopendekezwa ni lazima awe mkazi husika, awe mlipaji mzuri wa maji na awe na elimu ya kidato cha sita au diploma.
Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Songea Mjini Mwinyi Msolomi amewataka madiwani wote kuandaa kikao cha tathimini ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa muda wa miaka mitano 5 ili kubaini changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Msolomi ametoa Rai kwa Maafisa Watendaji kata wote na mitaa kuunda kamati za ulinzi na usalama kwenye maeneo yao ili kuzuwia matukio ya wizi hususani wizi wa ng’ombe ambao unaripotiwa mara kwa mara kutoka kwa wananchi.
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
MANISPAA YA SONGEA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa