Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano amefanya ziara ya kutembelea miradi ya afya inayoendelea kujengwa katika kata ya Tanga, Lilambo, pamoja na kata ya Mletele.
Ziara hiyo imefanyika kwa siku tatu 3 kuanzia tarehe 06 juni 2023 hadi 08 Juni 2023 ambapo alifanikiwa kutembelea kituo cha afya Lilambo kilichoojengwa kwa thamani ya Mil. 550 fedha za mapato ya ndani na kimeanza kutoa huduma za awali, Kituo cha afya Mletele kinachojengwa kwa thamani ya Mil. 545 fedha kutoka Global Fund, pamoja na ujenzi wa Hospital ya Manispaa ya Songea inayojengwa kwa thamani ya Bil. 1 fedha kutoka Serikali kuu.
Mhe. Mbano “ametoa shukrani kwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha kiasi cha Bil 4 kwa lengo la kupunguza kero ya umbali wa upatikanaji wa huduma za Afya.”
Aliongeza kuwa, kituo cha afya Mletele kimegharimu jumla ya kiasi cha fedha Mil. 845 fedha ambazo Mil 545 zimetumika kwajili ya ujenzi na Mil 300 kwa ajili ya vifaa tiba ambapo ujenzi utakamilika mara ifikapo tarehe 30 juni 2023.
Imeandaliwa na;
Amina Pilly;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa