BILIONI 14 KUJENGA BARABARA ZA LAMI MANISPAA YA SONGEA
ZAIDI ya sh.bilioni 14.320 zinatarajiwa kutumika katika wa ujenzi wa barabara za mji wa Songea katika kiwango cha lami zenye urefu wa kilometa 8.6.
Fedha za mradi huo zimetolewa na Benki ya Dunia chini ya Mpango wa kuzijengea uwezo serikali za mitaa(ULGSP), mpango huo unakusudia kuendeleza miundombinu ya Halmashauri za miji na manispaa 18 za Tanzania Bara ikiwemo Manispaa ya Songea.
Mradi huo ambao ulianza Juni Mosi 2015 ulitarajiwa kukamilika Juni 30,2017 ambapo fedha iliyopokelewa na Manispaa ni zaidi ya sh.bilioni saba ambapo hadi sasa Mkandarasi ameshalipwa zaidi ya sh.bilioni nne.
Barabara za Manispaa ya Songea ambazo zipo kwenye mradi huu ni FFU hadi Matogoro yenye urefu wa kilometa 3.2,barabara ya Songea Girl’s hadi Mateka yenye urefu wa kilometa 1.5 na barabara ya Mwembechai hadi Bombambili yenye urefu wa kilometa 2.6.
Barabara nyingine ni Mitumbani hadi Yapenda yenye urefu wa kilometa moja,barabara ya Polisi hadi Stendi ya Mlilayoyo yenye urefu wa kilometa 0.45.
Hata hivyo muda wa kumaliza kazi kwa Mkandarasi ulimalizika tangu Juni 30 mwaka huu ambapo tayari Mkandarasi huyo ameingizwa kwenye tozo(Liquidated Damage) na kwamba iwapo atashindwa kumaliza kazi kwa siku 100 hatua za kisheria za kuvunja mkataba zitafanyika.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa