SERIKALI mkoani Ruvuma imewapongeza watawa wa shirika la Mtakatifu Agnes Chipole Jimbo kuu katoliki la Songea kwa kuanzisha fursa nyingine ya uwekezaji ambapo hivi sasa Bwawa la uzalishaji umeme wa maji la Tulila lililopo katika kata ya Mpepai wilayani Mbinga , limeanza kutumika kama kivutio cha utalii.
Mkurugenzi wa Mradi wa umeme wa maji wa Tulila Sr. Yoela Luambano amesema watawa hao wameanzisha utalii wa kuangalia ndege adimu,pia kuna utalii wa kusafiri kwa boti , kuangalia wanyama kama viboko,mamba na samaki waliopo katika Bwawa hilo ambalo linatokana na maporomoko ya Maji ya mto Ruvuma.
Watawa wa Chipole ndiyo wamiliki wa mradi wa umeme wa maji wa Tulila ambao unaotumika katika mji wa Songea.
Imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Oktoba 19,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa