Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho, akiwa ameambatana na Kamati ya Siasa ya Mkoani hapa, ameridhishwa na Utekelezaji wa miradi ya Maendeleo na ushirikishwaji wa jamii katika miradi iliyotekelezwa kwa mwaka wa fedha 2018/2019 katika Wilaya ya Nyasa.
Ameyasema hayo jana wakati akihitimisha Ziara ya kikazi siku mbili agosti 14-15, ya kutembelea na kukagua, miradi ya maendeleo katika Tarafa ya mpepo na Luhekei, Wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma.
Bwana Mwisho alifafanua kuwa kwa Miradi nane(8)ambayo amekagua amefurahi kuona imetekelezwa vizuri na kwa kiwango cha hali ya juu, na Jamii imeshirikishwa na wanatambua miradi yote inayotekelezwa katika maeneo yao, na wanachangia nguvu zao licha yaSerikali kutoa Fedha ili kuunga Mkono juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Aliitaja miradi aliyokagua kuwa nia Ujenzi wa Hosteri mbili shule ya Sekondari Kingerikiti,Ukamilishaji wa vyumba 3 vya madarasa shule ya msingi Kibaoni,iliyopo Kata ya Tingi ambayo iko hatua ya Ring bim, Ujenzi wa Vyumba nane vya madarasa,matundu sita ya vyoo,meza 240 na viti 240 na ujenzi wa bw Sekondari Mhandisi Stella Manyanya katika Kata ya Mpepo Wilayani hapa.
Aliongeza miradi minginwe aliyokagua nia Shamba la Miti ya Misindano (Pines Patula) iliyopandwa na Wakala wa huduma za Misitu Tanzania shamba ambalo lina ukubwa wa Hekta 20,905 zinazofaa kwa ajili ya upandaji miti na hekta 680 kati ya hizo zimetumika kwa kupandwa miti 555,500/= na upanuzi wa shamba ukiwa unaendelea,mradia ambao ulimfurahisha sana na kutoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Ruvuma wapande miti ili kutunza mazingira na kuongeza kipato kwa wananchi kwa miaka ijayo.
Pia alikagua ujenzi wa hosteri na bwalo la Chakula shule ya Sekondari Nyasa katika Kata ya Chimate na Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Nyasa ambayo imefikia Asilimia tisini na tano(95) ya ukamilishaji, wa majengo saba yanayojengwa katia Kijiji Cha Nangombo Kata ya Kilosa Wilayania hapa na alitoa Pongezi Kwa ushirikiano mzuri uliopo kati ya Wananchi,wataalam na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela Chilumba,
“Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Uongozi wa Wilaya ya Nyasa ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela Chilumba na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa Bw.Jimson Mhagama kwa ushirikiano mliouonyesha katika Ujenzi wa Hospitali hii ya Wilaya ambayo imejengwa kwa Ustadi mkubwa na ushirikiano wa hhli ya juu kati ya Wananchi wataalam na Serikali.Naomba ushirikiano huu uendelee.
Miradi mingine aliyoikagua ni ujenzi wa Ofisi ya Mdhibiti wa Elimu Wilaya ya Nyasa na Ujenzi wa jengo la Tanesco lilopo katika kijiji cha kilosa na Kata ya KIlosa wilaya ni hapa.
Aidha alitoa wito kwa Viongozi wote wa Chama cha Mapinduzi(CCM) kuanzia ngazi ya Shina, Tawi, Kata Wilaya na Mkoa kuhakikisha wanawahamasisha wananchi kushiriki shughuli mbalimbali za miradi ya maendeleo zinazotekelezwa katika Maeneo yao.
Imeandaliwa Na Netho c.Sichali ofisa habari,wilaya ya Nyasa,0767417597
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa