WAGOMBEA kupitia Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Ruvuma wameshinda nafasi zote za viongozi serikali za mitaa bila kupingwa kwa asilimia 100.
Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma Nuru Ngeleja amesema CCM imeshinda viti katika vijiji vyote 551 mkoani Ruvuma,mitaa yote 124 na vitongoji vyote 3723.
“Wagombea wote wa CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2019,wameonesha kukubalika ndani nan je ya CCM hali ilisababisha kushinda bila kupingwa kwa asilimia 100’’,alisisitiza Ngeleja.
Hata hivyo Katibu Mkuu huyo wa CCM amesema kabla ya mapingamizi na rufaa,Chama cha Mapinduzi mkoani Ruvuma viongozi wake walishinda kwa asilimia 75.
Amesema ushindi huo unaonesha imani kubwa waliokuwa nayo watanzania ndani na nje ya CCM pamoja na watanzania wasiokuwa na vyama na kwamba hali hiyo imetokana na kazi kubwa inayofanywa na serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli.
Amesema hata kama watajitokeza watu wa kupotosha,ukweli utabaki wazi kwa sababu kazi za kuwaletea maendeleo watanzania zinaonekana na kila mmoja katika sekta mbalimbali ikiwemo miundombinu,afya,umeme,maji na elimu.
Imeandikwa na Albano Midelo
Novemba 15,2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa