Hayo yamebainika jana tarehe 20/02/2020 katika kikao cha Baraza la madiwani manispaa ya Songea kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
Baraza hilo, likiongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Alhaj Abdul Hassan Mshaweji, akisema “Manispaa ya Songea Inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo na ubovu wa miundombinu ya Barabara za mitaa ambapo amesema “katika mwaka wa fedha 2019/2020 serikali imetenga fedha Zaidi ya tsh Bil 1,398 katika kufanyia matengenezo ya mtandao wake wa barabara.
Naye Kaimu Maneja wa TARURA Manispaa ya Songea Eng Henry Mtawa “alisema bajeti iliyopitishwa kwa ajili ya matengenezoya BaraBara kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ikiwa kwa ajili ya matengenezo ya barabara za mita zilizoko Manispaa ya Songea, jumla ya km 520.70 kati ya hizo km 256.69 ni za mjazio, km 261.94 ni za mkusanyo na km 2.07 ni za jamii/ Kijiji.”
Aidha, alizitazja changamoto zinazoikabili TARURA ni; ufinyu wa bajeti ya Matengenezo ya Barabara na amezitaja njia za utatuzi wa changamoto hizo ni pamoja na Bajeti ya matengenezo ya barabara iongezwe ili kuendana na uhalisia wa mahitaji ya matengenezo.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KAIMU AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa