MKUU wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Pololet Mgema amekiri wilaya ya Songea inakabiliwa na changamoto ya elimu bila malipo hali ambayo imesababisha baadhi ya shule za msingi na sekondari kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi.
Amesema utekelezaji wa elimu bila malipo umesababisha ongezeko kubwa la wanafunzi walioandikishwa darasa la kwanza na wanaojiunga kidato cha kwanza hali iliyosababisha upungufu wa vyumba vya madarasa na madawati.
Hata hivyo amesema hivi sasa kazi ya kutengeneza madawati na ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa inaendelea .
Afisa Taaluma Sekondari wa Manispaa ya Songea Flowin Komba amezitaja shule za sekondari zenye upungufu mkubwa wa vyumba vya kusomea,viti na meza kuwa ni Msamala, Bombambili,Londoni,Matarawe na Mfaranyaki.
Imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa