MKUU wa wilaya ya Songea ametoa rai kwa viongozi wa dini,wazazi,walezi na jamii kwa ujumla kuacha upotoshaji kuhusu chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi ambayo imeanza kutolewa leo Aprili 23 nchini kote ambapo kwa kuanzia watoto wa kike wenye umri wa miaka 14 wanaanza kupewa chanjo hiyo.
Manispaa ya Songea inatarajia kutoa chanjo ya mlango wa kizazi kwa wasichana 1834 ambapo lengo la Mkoa wa Ruvuma ni kutoa chanjo hiyo kwa wasichana 28,676.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dk.Gosbert Mutayabara anautaja ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi na matiti kuwa ni miongoni mwa magonjwa kumi katika mkoa wa Ruvuma yanayoongoza kwa kusababisha vifo.
Takwimu za saratani za mlango wa kizazi na matiti katika mkoa wa Ruvuma zinaonesha kuwa mwaka 2014 kulikuwa na wagonjwa zaidi ya 12,000,mwaka 2015 wagonjwa zaidi ya 17,000 na mwaka 2016 wagonjwa wa saratani walikuwa zaidi ya 18,000.
Takwimu zinaonesha kuwa kila mwaka wagonjwa 6000 wa saratani za mlango wa kizazi na matiti wanagundulika kati yao wagonjwa 4000 wanapoteza maishaKulingana na takwimu za Ocean Road,saratani za mlango wa kizazi na matiti husababisha asilimia 50 ya vifo vyote vinavyotokana na saratani kwa akinamama.Utafiti unaonesha kuwa akinamama karibu 500,000 hupatwa na ugonjwa wa saratani ya uzazi na matiti kila mwaka duniani, kati ya hao akinamama 250,000 hufariki kila mwaka kutokana na ugonjwa huo.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa