CHUO pekee kinachotoa mafunzo ya Ufamasia katika ukanda wa Kusini kimeanzishwa katika Kata ya Msamala Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Mkurugenzi wa Kampuni ya TOPONE LIMITED ambao ndiyo wamiliki wa Chuo hicho Pascal Msigwa amesema chuo hicho kinatarajia kufunguliwa Oktoba mwaka huu ambacho kwa kuanzia kitakuwa kinatoa mafunzo ngazi ya cheti ambayo yanachukua miaka miwili.Msigwa amesema chuo hicho kimesajiriwa na Baraza la Ufundi la Taifa (NACTE) na kupewa namba ya usajiri 184 na kwamba lengo la kuanzisha chuo hicho kuiunga mkono serikali ya Awamu ya tano ya kuzalisha watalaamu wa ufamasia hapa nchini ili kukabiliana na upungufu uliopo.
Kwa upande wake Mratibu wa Mafunzo ya Chuo hicho David Anderson amesema chuo hicho kinafaa vyote muhimu ambavyo vitatumika kwa wanachuo ikiwemo maabara yenye vifaa vya kutosheleza,maktaba,vyumba vya madarasa na mabweni.Hata hivyo amesema kwa kuanzia chuo hicho kinatarajia kuchukua wanachuo wasiozidi 200 na amezitaja sifa za kujiunga na chuo hicho ni wanafunzi waliomaliza kidato cha nne waliofaulu katika kiwango cha chini ni ufaulu wa D nne kati ya hizo D mbili katika masomo ya Sayansi Biolojia na Kemia na D nyingine mbili katika masomo mengine isipokuwa masomo ya Dini na Biashara.
Amelitaja lengo la chuo hicho ni kutoa elimu bora na kufanya utafiti katika masuala ya dawa ili kutoa majibu sahihi kwa jamii kutokana na utafiti huo uliofanywa katika ufamasia.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Septemba pili,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa