Kifungu cha 10 (1) (C ) cha sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Na. 2 ya mwaka 2024 ambacho kinaelekeza kwamba Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi itasimamia Uchaguzi wa Serikakali za Mitaa kwa kutumia Sheria itakayowekwa.
Hayo yamejiri wakati wa kufungua mkutano wa Tume na maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri zote Nchini uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Saalam jana tarehe 15 Juni 2024 kwa lengo la kutoa taarifa za uwepo wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura pamoja na kuelekeza namna ya utumiaji wa vifaa na mfumo wa uandikishaji utakavyotumika kwenye vituo vya uandikishaji daftari la wapiga kura.
Akifungua Mkutano huo Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi NEC, Ndugu Ramadhani Kailima amesema” Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri wanatakiwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kujiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga Kura.”
Amewataka Maafisa Habari hao kutumia njia mbalimbali katika kuelimisha jamii kuhusu kujiandikisha kwenye daftari la Wapiga ambalo kwa awamu ya kwanza zoezi hilo linatarajia kuanza tarehe 01 Julai 2024.
Akizungumza Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Bi Giveness Aswile amebainisha kuwa kwa kuzingatia sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 Daftari linatatrajiwa kuwa na wapiga kura 34,746,638 kutoka 29,754,699 ya mwaka 2020 ambalo ni ongezeko la wapiga kura wapya 5,586,433 sawa na 18.7%.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa