Na,
AMINA PILLY,
AFISA HABARI MANISPAA.
14.04.2022
Wakala wa barabara za vijijini na Mjini (TARURA) Wilaya ya Songea kuanza kujenga upya daraja la Matarawe hadi Mjimwema ifikapo Aprili 15, 2022.
Hayo yamebainishwa na Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TARURA hapo jana tarehe 13 Aprili 2022.
Mbano alisema kuwa kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mkoani Ruvuma ambazo zimesababisha kuvunjika kwa daraja la Matarawe - Mjimwema na kuleta madhara katika shughuli za usafirishaji kwa watumiaji wa barabara hiyo.
Hivyo, kuanzia tarehe 15 Aprili 2022 barabara hiyo itafungwa rasmi kwa ajili ya matengenezo katika kipindi cha siku 60 ambapo amewataka wananchi kuwa wavumilivu kwa kipindi hicho chote cha matengenezo.
Naye Meneja wa TARURA Wilaya ya Songea Eng. John Ambrose alisema kuwa wamepokea fedha kutoka Serikalini kwa ajili ya matengenezo ya dharura ya daraja hilo na zoezi la ujenzi litaanza rasmi kuanzia Aprili 15, 2022, hivyo amewataka wananchi kutumia njia mbadala wakati wa ujenzi wa daraja hilo hadi hapo ujenzi utakapokamilika.
Aliongeza kuwa daraja litakalojengwa hivi sasa litakuwa na uwezo wa kupitisha gari la mzigo lenye uzito usiozidi TAN 15.
Mwisho.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa