Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela Chilumba hivi karibuni ameweka jiwe la msingi katika Mradi wa Maji unaotekelezwa katika Kijiji cha Liparamba Kata ya Liparamba, Wilayani Nyasa ambao utawanufaisha wakazi 4694. Mpaka kukamilika kwake.
Katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi uliofanyika katika viwanja vya Kituo cha Afya cha Liparamba Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabeba Chilumba alimuagiza Mkandalasi anayetekeleza mradi huu kukamilisha kwa wakati na kuhakikisha maji yanatoka kabla ya mwezi wa tisa kama mkataba unavyosema.pia aliwaagiza wananchi waitunze miundombinu inayojengwa na Serikali kwa ajili ya kutatua kero ya maji iliyowasumbua kwa muda mrefu.
Aliongeza lengo la Serikali ni kutatua kero zinazowakabili wananchi wake ili waweze kufanya shughuli za kimaendeleo kama alivyohakikisha kata ya Liparamba inapata maji safi na salama.
“Nakuagiza Mkandarasi wa mradi huu ufanye kazi kwa juhudi usiku na mchana na ifikapo mwezi Septemba uwe umemaliza na maji yatoke ili yatatue kero kwa wananchi wa kata hii ya Liparamba.Pia ninawaagiza wananchi muitunze miundombinu ya maji kwa kuhakikisha jumuiya za watumia maji zinatekeleza majukumu yao”
Awali akisoma taarifa ya maendeleo ya mradi huo,Kaimu Meneja wa wakala wa maji mijini na vijijini JosephatKayumba alisema mradi umefikia asilimia 85 ya utkelezaji na unatekelezwa na Mkandarasi wa kampuni ya Ovansi Contruction Limited, iliyoshinda Zabuni ya kujenga mradi, kwa gharama ya shilingi (1,020,089,315.00) ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa sekta ya maji awamu ya pili , (WSDP II) Nchini Tanzania ambao ulianza kutekelezwa mwaka wa fedha 2015/2016.
Alizitaja kazi zilizofanyika kuwa, ni kujenga miundombinu ya vyanzo viwili vya maji (intakes) na sehemu moja ya kukusanyia maji, kujenga tanki la kutunzia maji lenye ujazo wa mita sabini na tano (75m3) na Mtandao wa mabomba, ya kusambaza maji kilometa ishirini na tano (25.85) .Pia amejenga vituo vya kuchotea maji ishirini na tisa(29) na matanki madogo ya kupunguza msongo wa maji katika bomba sita (6)chemba thelathini na saba (37) katika maeneo mbalimbali ya mradi, pamoja na alama za bomba.
.
Wananchi wa kijiji cha Liparamba, wamefurahi kutatuliwa kero ya maji kwa kuwa awali walikuwa wakitembea umbali wa kilometa takribani tano kufuata maji huduma ya maji . kituo cha afya kilikuwa hakina maji hali iliyokuwa inawapa shida wagonjwa na wauguzi kutafuta maji wapatapo changamoto ya kuugua au kuuguliwa. Kwa sasa wanaipongeza Serikali kwa kuwatatulia kero ya maji katika kijiji chao.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kata ya Liparamba Diwani wa Kata hiyo Ditram Nchimbi aliishukuru Serikali kwa kutatua kero ya maji katika kata hiyo na kusema watahakikisha wanaitunza miundombinu ya maji kwa kupanda miti rafiki maji na kuhakikisha vikundi vya watumia maji vinafanya kazi wakati wote.
“Mh Mkuu wa Wilaya tunaishukuru sana Serikali kwa kuhakikisha inatatua changamoto ya maji katika kijiji chetu kwa kuwa Wananchi walikuwa wakiteseka sana kutafuta maji kwa kuwa walikuwa wanatembea umbali wa Kilometa takribani tano kutafuta maji.Tutahakikisha tunaitunza Miundombinu kwa kuhakikisha jumuiya ya watumia maji zinafanya kazi muda wote”Alisema Nchimbi.
Serikali imetoa shilingi bilioni moja na nusu kwa ajili ya kutekeleza mradi mkubwa wa maji katika kata ya Liparamba wilayani hapa ili kutatua changamoto ya maji iliyokuwa inawakabili wakazi hao.
Imeandikwa na Netho Credo
Afisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa