Na,
AMINA PILLY,
AFISA HABARI MANISPAA.
05.11.2021
Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema ameendelea na ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19, miradi ambayo inaendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ndani ya Manispaa ya Songea hapo jana tarehe 9 Novemba 2021.
Mgema ameendeleaa kufanya ziara hiyo kwa lengo la kukagua maendeleo ya utekelezwaji wa miradi hiyo ili kuhakikisha hadi kufikia muda maalumu uliopangwa na Serikali ambao ni tarehe 15 Disemba 2021 miradi yote hiyo inatakiwa kukamilika.
Amesema kuwa utekelezaji wa miradi hiyo unaendelea vizuri ambapo hadi sasa ujenzi upo katika hatua ya madirisha hali ambayo inaonyesha miradi yote itakamilika ndani ya muda uliopangwa.
Miongoni mwa miradi aliyotembelea ni pamoja na ujenzi wa darasa 1 katika shule ya sekondari Mbulani, ujenzi wa madarasa 2 shule ya sekondari Luwawasi, ujenzi wa darasa 1 shule ya sekondari London, ujenzi wa madarasa 2 shule ya sekondari Mletele, ujenzi wa madarasa 2 shule ya sekondari Mashujaa, ujenzi wa ukuta katika shule ya sekondari Mateka, ujenzi wa madarasa 2 shule ya sekondari Ruvuma, ujenzi wa madarasa 2 shule ya sekondari Chandarua pamoja na ujenzi wa bwalo la wanafunzi shule ya sekondari Emmanuel Nchimbi.
Mwisho.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa