Na
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
14.10.2021
Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema amewataka watumishi na wananchi kujijengea tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara ili kujenga afya bora ya mwili.
Hayo yamebainishwa leo tarehe 14 oktoba 2021 katika uwanja vya michezo Zimanimoto katika kuadhimisha Siku ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere ambaye hadi sasa ametimiza miaka 22 toka afariki dunia.
Maadhimisho hayo Kitaifa yamefanyika Wilaya ya Chato Mkoani Geita ambapo katika kuunga mkono maadhimisho hayo, Wilaya ya Songea yameadhimishwa kwa kushiriki kufanya mazoezi ya viungo vya mwili iliyofanyika katika uwanja wa Zimanimoto Manispaa ya Songea ambapo pia ameagiza kuendelea kufanyika kwa mazoezi hayo kila baada ya wiki ya pili ya mwanzo wa mwezi husika.
Pololet alisema “ tunatambua mchango mkubwa uliotolewa na Baba wa Taifa katika kukomboa Nchi ya Tanzania” hivyo tunapaswa kukumbuka kifo chake pia kuhakikisha tunatii yale yote aliyofanya ikiwemo na kufanya uzalendo pamoja na kujifunza kujitegemea. Alisisitiza.
Aliongeza kuwa “nanukuu “Kazi ni kipimo cha utu hivyo Mwl Nyerere alihimiza kujitegemea kwa kufanya kazi kwa bidii na kuwa sehemu ya mchango wa kujenga Taifa letu” . mwisho wa kunukuu.
Alisema kuwa Mwl Nyerere ni mwanamapinduzi wa Bara la Afrika ambaye alipenda kutenda haki, alipinga dhuluma, na lisisitiza kila mmoja apiganie haki yake ili kila mmoja aweze kujikomboa.
Nchi yetu ilipopata uhuru Mwl Nyerere alitamka kuwa “ Uhuru wetu hautakuwa na maana kama majirani zetu wanaotuzunguka hawatakuwa na Uhuru”, Hivyo hatuna budi nasi kuwapenda majirani zetu ili kujenga uhusiano bora katika jamii.
Pololet amewataka wananchi wilayani Songea kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa UVIKO 19 sambamba na kuvaa barakoa, kutumia vitakasa mikono, pamoja na kuchoma chanjo ya UVIKO 19 ambayo inapatikana bure katika vituo vyote vya afya.
Mwisho
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa