MKUU wa wilaya ya Songea Pololet Mgema amekabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 71 zilizotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Songea Kama mkopo kwa vikundi 53 kwa ajili ya kuendeleza miradi Yao.
Vikundi hivyo vinafanya miradi ya ufugaji wa ng’ombe,kuku wa mayai,ufugaji wa samaki na miradi mingine.
Halmashauri ya manispaa ya Songea kupitia mapato yake ya ndani imekuwa inatoa mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali vya vijana na wanawake.
Afisa Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Manispaa hiyo Naftari Saiyoloi anasema kupitia mapato yake ya ndani Manispaa hiyo katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha wa 2017/2018 imetenga zaidi milioni 188 kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya wanawake na vijana.
Anasema kati ya fedha hizo milioni 170 zimelenga kukopesha vikundi 177 ambapo asilimia 10 ya fedha hizo ambazo ni sawa na milioni 18 zitatumika katika usimamizi na ufuatiliaji wa mrejesho.
Kulingana na Saiyoloi katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha wa 2017/2018 Halmashauri ya Manispaa imewezesha vikundi vya wajasirimali sh.milioni 83 kati ya hizo milioni 66 tayari zimekwishaandaliwa kwa ajili ya kukopesha wanawake na vijana.
Anabainisha kuwa shilingi milioni 17 zitakopeshwa baada ya mchakato wa kutambua vikundi stahili vya kukopeshwa kukamilika katika Halmashauri ya Manispaa hiyo.
Hafla hiyo ambayo imefanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea pia imehudhuriwa na Mstahiki Meya Abdul Hassan Mshaweji na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Mhandisi Samwel Sanya.
Taarifa imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa