“Songea tunasonga mbele”
Kauli hiyo imetamkwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema katika kikao kazi na wakuu wa Idara, Maafisa Watendaji wa Kata, Maafisa Watendaji wa Mitaa kwa ajili ya kupanga mkakati wa kumaliza kugawa vitambulisho vilivyobakia 8873 vya wajasiliamali wadogo, kilichofanyika leo 27.11.2020 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Kamando alisema “kwa mwaka 2019 Manispaa Ilipokea vitambulisho vya ujasiliamali wadogo 11,000 ambavyo kwa jitihada nzuri za watendaji hao waliweza kukamilisha kuvigawa kwa wakati nakuifanya Halmashauri ya Manispaa ya Songea iwe ya kwanza kimkoa wa Ruvuma kwa utekelezaji mzuri” aliwapongeza.
Aliongeza kuwa mwaka huu 2020 Manispaa imepokea Vitambulisho 11,000 ambapo hadi hivi sas vitambulisho vilivyogawiwa ni 2127, ambavyo havijagawiwa ni 8873 ambapo amesema haoni sababu ya msingi ya kutomaliza kutekeleza zoezi hilo.
Amewataka wataalamu hao kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha kila mkuu wa Idara na Vitengo, Maafisa wa Watendaji kata na mitaa wanasimamia na kushiriki kwenye zoezi hilo kikamilifu ili kufikia lengo lilikubalika.
Amewataka wataalamu hao kufanya kazi kwa kushirikiana (timu), na bila kuwanyanyasa wajasiliamali hao ili kufanikisha zoezi la ugawaji wa vitambuliusho kwa wajasiliamali wenye sifa.
Lengo kuu la Serikali kuwawezesha wajasiliamali wenye mitaji midogo kukuza mitaji yao kwa kuondoa ushuru wa shilingi mia nne 400 ambao hutozwa kila siku na kulipa shilingi elfu ishirini 20,000 ambayo hulipwa mara moja ndani ya mwaka husika. Pololet alibainisha.
Naye Afisa biashara Manispaa ya Songea Furaha Mwangakala alisema miongoni mwa mikakati waliyojiwekea ili kufikia lengo ni pamoja na kufanya kazi kwa timu na kwa kushirikiana na wakuu wa idara na vitengo, kila mtendaji wa kata /Mtaa kuhakikisha anashiriki zoezi hilo, pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa jamii umuhimu wa kununua kitambulisho cha mjasiliamali.
Amewataka wataalamu hao kuanza kazi mara moja ya ugawaji wa vitambulisho pamoja na kufanya uhakiki kwa kila mjasiliamali kama ana kitambulisho cha ujasiliamali na kama hana kitambulisho anapaswa kununua kitambulisho au kukata leseni ya biashara.
MTAYARISHAJI;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
27.11.2020.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa