Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema ametoa onyo kwa wafanyabiashara wanaotumia vipimo batili kwa lengo la kuwaibia wananchi.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wakati akifungua semina iliyoandaliwa na wakala wa vipimo Mkoa wa Ruvuma ambayo imelenga kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya vipimo kwa wafanyabiashara mbalimbali iliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa Songea tarehe 05.05.2021.
Pololet amebainisha kwamba kumekuwa na matumizi makubwa ya vipimo batili katika meneo ya biashara hususani kwenye masoko makubwa ambapo asilimia kubwa ya wafanyabiashara wamekuwa wakitumia vipimo visivyo rasmi na hivyo huwaibia watumiaji wa huduma hizo.
Amewataka wakulima na wafanyabiashara kuacha kutumia vipimo batili kama dumla,makopo, ndoo na lita ili wakulima na jamii kwa ujumla wapate tija yenye thamani sawa na uzalishaji wao, na yeyote atakayebainika kukiuka agizo hilo hatua kali itachukuliwa ‘Pololet alisisitiza’
Aidha ameagiza mamlaka zinazohusika na usambazaji wa maji (RUWASA na SOUWASA) kuhakikisha kwamba wanafungia wateja wao mita ambazo tayari zimehakikiwa na wakala wa vipimo Mkoa wa Ruvuma
Ameipongeza taasisi ya wakala wa vipimo kwa kuongeza maeneo mapya ya ukaguzi ili kupanua wigo na kumlinda mlaji kutokana na matumizi sahihi ya vipimo, pia umetolewa wito kwa Wananchi kuzingatia matumizi ya vipimo sahihi kwa sababu kipimo ni muhimu katika maisha ya kila siku.
Naye Kaimu Meneja wakala wa vipimo Mkoa wa Ruvuma Nyagabona Edward Mkanjabi amesema kwamba mafunzo hayo yametolewa ili kuelimisha jamii juu ya matumizi sahihi ya vipimo na kuachana na vipimo batili ‘Alisisitiza’.
Baadhi ya wafanyabiashara walioshiriki semina hiyo wamepongeza wakala wa vipimo Mkoa wa Ruvuma kwa kuwapa elimu juu ya matumizi sahihi ya vipimo ambayo yatawasaidia kuwanufaisha wao na watumiaji wa huduma zao.
IMEANDALIWA NA,
AMINA PILLY,
AFISA HABARI MANISPAA,
05.05.2020
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa