Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema amefanya ziara ya kushitukiza katika shule za Sekondari kwa ajili ya kufanya uhakiki wa wanafunzi walioripoti kidato cha kwanza sambamba na kuzungumza na walimu wa shule husika.
Elimu ni haki ya msingi ya kila mtoto hivyo kila mwanafunzi aliyechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2023 lazima aende shule ambapo amewataka maafisa Tarafa kusimamia zoezi la wanafunzi wasioripoti shule na taarifa hizo ziwasilishwe ofisi ya Mkurugenzi kila wiki.
Pololet aliongeza kuwa Serikali ya awamu ya sita inaendelea kufanya jitihada za kuongeza miundombinu ya kusomea, kutoa vifaa vya kufundishia ili kila mwanafunzi aweze kupata elimu bora kwa maendeleo ya Taifa la letu.
Hayo yametolewa jana tarehe 18 Januari 2023 ambapo alitembelea shule ya Sekondari Mashujaa, shule ya Sekondari Matogoro, Shule ya Sekondari Msamala, na Shule ya Sekondari Bombambili.
Amewataka wanafunzi kutekeleza wajibu wao ikiwemo na kushiriki vipindi vya masomo pamoja na kutenga muda wa ziada wa kujisomea wawapo majumbani mwao ili waweze kupata matokeo mazuri na kupandisha hali ya ufaulu kwa shule na Halmashauri husika
Akitoa Kauli mbiu ya NIACHE NISOME, kiongozi huyo ametoa Rai kwa wanafunzi kuachana na tabia ya kujiunga na makundi hatarishi ya utumiaji wa dawa za kulevya, kushiriki mapenzi umri mdogo ambayo hupelekea wasichana kupata mimba za utotoni ambazo huathiri masomo kwa watoto wa kike. “Pololet alikemea.”
Akibainisha hali ya kuripoti kwa wananfunzi wa kidato cha kwanza kwa shule ya Sekondari “Mashujaa alisema wanafunzi Pangiwa ni 309 kati ya hao walioripoti ni 172, Msamala Sekondari wanafunzi Pangiwa ni 773 walioripoti ni 397, Matogoro Sekondari wanafunzi pangiwa 232 walioripoti 263 kati yahao waliohamia 110 pamoja na shule ya Bombambili wanafunzi pangiwa 486 na walioripoti 353.”
Kwa upande wa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2023 ambao tayari wameshaanza masomo wametoa shukrani kwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hssan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha kwa ajili ya kujenga madarasa mapya kwa kila shule ya sekondari. “ Wameshukuru”
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWSASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa