Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe. Kapenjama Ndile amewataka viongozi kutoa ushirikiano kwa mwekezaji wa Bustani ya Manispaa Songea Hamza Mohamedy “ DELIGHT GARDEN PARK” ambayo imefunguliwa tarehe 22 Sepytemba 2023 na kuanza kutoa huduma.
Akizungumza kwenye tafrija hiyo Mhe. Ndile alisema” Hivi karibuni Serikali inaanza ujenzi wa barabara kutoka Muhukulu kwenda Magwamila pia na ujenzi wa kiwanda cha Miwa ambacho itawezesha kufungua fursa za kiuchumi na uwekezaji hususan katika mji wa Songea.
Hivyo, amewataka wananchi, na wadau mbalimbali kuwekeza katika maeneo ya ndani ya Songea ili kuleta maendeleo ya kiuchumi, uwekezaji, viwanda na fursa za kitalii.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Komredi Oddo Mwisho ametoa wito kwa Waheshimiwa Madiwani kuendelea kushirikiana na wataalamu na kuhamasisha wadau waweze kuja kuwekeza katika Maeneo mbalimbali ili kuleta maendeleo kwa wananchi wa Manispaa ya Songea.
Naye Afisa Biashara Joseph Martin Kabalo alisema “ Elimu iendelee kutolewa kwa wananchi juu ya uwekezaji ili kuweza kupata wadau wengi waweze kuwekeza katika maeneo mji wa Songea ikiwemo na hoteli.
Martin aliongeza kuwa Mil. 348 zimetumika katika uwekezaji huo ambao pia umesaidia kuongeza fursa za ajira kwa wananchi wa Manispaa ya Songea. “Alipongeza”
Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Songea Janeth Moyo alitoa pongezi kwa Mwekezaji Hamza Mohamedy “ DELIGHT GARDEN PARK” kwa kuwekeza katika Bustani hiyo ambayo itawezesha Halmashauri kupataa mapato.
Kwa upande wake Mwekezaji Hamza Mohamedy alitoa shukrani kwa Manispaa ya Songea kwa kumpatia eneo hilo kwa ajili ya uwekezaji ambapo amewataka viongozi, wananchi kumuunga mkono katika uwekezaji wake ambao amewekeza kwa gharama ya Mil. 348. “ alishukuru”
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa