Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro (MB) amewataka wananchi kuwa nasubira wakati ambao Serikali inaendelea kutatua changamoto zao za mipaka ya kata ya Mletele na Seedfarm ambayo imeshachukuliwa hatua za utekelezaji.
Amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Seedfarm, Mletele na Bombambili ambao umefanyika leo tarehe 09 Julai 2024 kwa lengo la kupokea na kutatua kero za wananchi wa kata hiyo, ambayo ilishirikisha timu ya wataalamu kutoka Manispaa ya Songea, TARURA, SOUWASA, TANROAD, TANESCO nA viongozi wa kamati ya Siasa Wilaya, Pamoja na Waheshimiwa Madiwani.
Ziara hiyo itafanyika kwa kata 21 ambapo kwa awamu ya kwanza ambayo ni leo tarehe 09 Julai ameweza kutembelea na kuzungumza na Wananchi katika kata 3 ambazo ni Mletele, Seedfarm, na Bombambili.
Imeandaliwa na;
Amina Pilly;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa