Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango amewataka wataalamu wa afya Nchini kote kuwa na uzalendo, uadilifu na kuzingatia maadili ya utumishi wakati wanapo hudumia wagonjwa.
Kauli hiyo imetolewa tarehe 21 julai 2023 akiwa katika uzinduzi wa kituo cha afya Lilambo kilichojengwa kwa Mil. 503 fedha za mapato ya ndani ambacho kimeanza kutoa huduma.
Dkt. Mpango amesema” Serikali imeendelea kusimamia Sekta ya afya katika kuboresha huduma za afya hususani kuongeza wataalamu wa afya kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi.
Amewataka kutunza miundombinu ya afya pamoja na utunzaji wa vifaa vilivyopo na kuhakikisha yanafanyika matengenezo ya miundombinu ya mara kwa mara ikiwemo na matumizi sahihi ya dawa kwa wagonjwa.
Ametoa rai kwa mawakala wa Pembejeo ya Ruzuku kuacha tabia ya kuwaibia Pembejeo wakulima, pia wakati wa kuuza mahindi wasiuze kwa kutumia vipimo visivyo rasmi (Rumbesa) ambavyo hupelekea kuwaibia wakulima.
Alisema Mkoa wa Ruvuma una bahati ya kupata mazao kwa wingi lakini ni mkoa ambao unaongoza kuwa na lishe duni hivyo amewataka akinamama wajawazito hadi kujifungua anatakiwa kula mlo wenye viini lishe ili kujenga lishe ya mama na mtoto anapozaliwa.
Kwa upande wake Waziri wa katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro alisema Kata ya Lilambo ina jumla ya Mitaa 8, yenye Zahanati 4, ndiyo maana wakaamua kujenga kituo cha afya ambacho leo kimefunguliwa.
Dkt. Ndumbaro alisema, Manispaa ya Songea imeendelea kutekeleza miradi mikubwa ikiwemo na Ujenzi wa Uwanja wa ndege wa kisasa ambao unachangi kipato kutoka kwa wageni ambao husafiri mara tatu kwa wiki, ujenzi wa chuo kikuu cha Uhasibu, ujenzi wa barabara KM 10.5 kuzunguka katikati ya mji, ujenzi wa barabar kutoka Makambako hadi Songea, miundombinu ya madarasa ya Elimu Msingi na Sekondari, pamoja na vituo 4 vya Afya na Hospitali ya Wilaya ambayo inaendelea kujengwa, na Hospital ya Rufaa ya Mkoa.
Akitoa shukrani kwa mgeni rasm alisema”Tarehe 22 Julai 2023 umekuja kuandika historia kwa kuja kuzindua Msaada wa Sheria wa Mama Samia Kampeni. “alishukuru”
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa