Picha mbalimbali za matukio ya ziara ya Dkt. Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipotembelea shule ya awali na Msingi ya Chief Zulu iliyoko Manispaa ya Songea, na kufanya uzinduzi wa shule hiyo ambayo imejengwa kwa fedha za mapato ya ndani Mil. 626.4 ambayo inafundishwa kwa lugha ya kiingereza isipokuwa kwa somo la kiswahili ambapo Shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 491.
Aidha akizungumza na wananchi mara baada ya kuzindua shule hiyo, mheshimiwa Rais ameahidi kutoa Mil. 100 kwa ajili ya ujenzi wa Bwalo la shule pamoja na ng'ombe wawili na kilo 500 za mchele pamoja na mafuta ya kupikia.
Imeandaliwa na;
Amina Pilly
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa