“Maadhimisho ya siku ya Uhuru 9 Desemba yatumike kwa kuelimisha jamii katika kuhifadhi tunu iliyowekwa na Wazee wetu.”
Kauli hiyo imetamkwa katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru 9 Desemba ambayo ilifanyika kiwilaya katika Ukumbi wa Manispaa ya Songea iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka Zanzibar, wataalamu, na viongozi kutoka Halmashauri ya Madaba, Songea Vijijini, na Manispaa.
Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea ambaye aliwakilishwa na Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano ambaye alisema “Lengo la maadhimisho haya ni kufanya Tafakuri na kukumbuka wapi tulipo na wapi tunatoka ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ambayo inamtaka kila mwananchi kulinda uhuru wetu.”
Mhe. Mbano alibainisha kuwa jukumu la kulinda Uhuru ni la kila mmoja wetu kwa kuwa Uhuru unalindwa kwa kufanya kazi kwa maana changamoto za Mtanzania zitatatuliwa na Mtanzania mwenyewe, hivyo amehimiza wananchi kuwa na Uzalendo kwa maendeleo ya Taifa.
Maadhimisho hayo yamefanyika kwa Mdahalo ambao ulizungumzia masuala ya Siasa na Uongozi, Elimu na Afya, Miundombinu, Mahusiano, na Nishati, Biashara, viwanda na uwekezaji, kilimo na mifugo, Maji na Mazingira.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Dkt. Frederick Sagamiko amewataka wananchi kuwa na utamaduni wa kupenda kujisomea historia ambayo itasaidia kukumbuka utamaduni wa maisha yetu ambao inaonesha watu walio wengi hupenda kufundishwa sio kujifunza.
Dkt. Sagamiko aliongeza kuwa nanukuu “ kuna mambo mengi sana yanakwenda kupotea kutokana na tabia yakutokuwa na utamaduni wa kufuatilia uhalisia wa kabla ya uhuru ambao jamii imekariri baadhi ya matukio muhimu ya kitafa ya kihistoria kama upatikanaji wa maji, viwanda.”mwisho wa nukuu.
Alisema hapo awali huduma hazikuwa nzuri kutokana na kutawaliwa na waingereza ambapo walitutumia kwa lengo la kuwatumikia wao katika kuzalisha mali hali ambayo hupelekea jamii kutopenda vitu vitokanavyo na asili yetu hali inayosababisha kuuwa viwanda vya ndani.” Alibainisha”
Hivyo ametoa Rai kwa wananchi wa Songea kuelekea maadhimisho yajayo ya 62 mwaka 2023 kuwepo kwa Makala inayoelezea maisha yetu kabla ya Uhuru na baada ya uhuru ambapo itasaidia kuweka kumbu kumbu katika maandishi ili kulinda historia na kurithisha kizazi kijacho. Dkt. Sagamiko alisisitiza.
Alibainisha kuwa kwa Manispaa ya Songea mara baada ya Uhuru imefanya shughuli nyingi sana ikiwemo na kuboresha miundombinu ya barabara za mitaa, miundombinu ya shule za msingi na Sekondari, UJenzi wa masoko mawili ya kisasa (Manzese) ambayo yanatarajia kutangazwa kwa ajili ya kuanza ujenzi hivi karibuni, ujenzi wa chuo kikuu cha hesabu (Arusha) ambapo imetengwa shilingi Bil. 17, Maji, Umeme, na Stendi kuu ya Mabasi Songea, ujenzi wa kiwanda kidogo Lilambo, ujenzi wa barabara wa kiwango cha Lami km 10.5 katika kata Mfaranyaki, Majengo, Misufini na Mjini naujenzi wa hosptali ya Rufaa ya Mkoa, Ujenzi wa vituo vya afya, ujenzi wa hosptali ya Wilaya iliyopo kata ya Tanga na nyinginezo.
Aliongeza kuwa Jukumu la Serikali ni kuweka miundombinu wezeshi kwa wafanyabiashara hususani katika kuwapanga wamachinga na sio dhamira ya Serikali kuuwa biashara bali Serikali inalenga kuwaweka huru wafanyabiashara wadogo.
Amewataka Maafisa watendaji wa kata na Mitaa kuwepo kwenye maeneo yao ya kazi na kuhakikisha wanasimamia zoezi la kuwapanga wamachinga kuwepo kwenye maeneo rasmi yaliyopangwa na Halmashauri.
Naye Juma Nyumayo (MDAU) alisema Uhuru ni hali au uwezo wa kujitawala au uwezo wa kutekeleza majukumu, kufanya maamuzi ya kushughulikia masuala yako wewe/ yenu bila kuwa chini ya Mamlaka nyingine.
Nyumayo aliongeza kuwa Mifumo ya Sheria za wakoloni za makosa jinai, ambazo hutumika Tanzania zilipokelewa kutoka kwa Waingereza pamoja na Mifumo ya Mahakama.
Naye Furaha Mwangakala alisema kabla ya uhuru Wilaya ya Songea hatukuwa na kiwanda, Soko, na Uwekezaji ambapo biashara nyingi zilifanywa na wageni kwa kuchukua bidhaa na kubadilishana bidhaa kwa bidhaa.
Mwangakala aliongeza kuwa Kabla ya uhuru Wilaya ya Songea ilikuwa na maduka mawili 2 ambapo baada ya uhuru Wilaya ya Songea ina jumla ya wafanyabiashara 14,260 kati ya hao wafanyabiashara wakubwa 3360 na wafanyabiashara wadogo ni 10,700.
Naye Afisa Mazingira Beno Philipo alisema Huduma ya maji Manispaa ya Songea ilianza mwaka 1950 kabla ya uhuru ambapo wakati Nchi inapata Uhuru 1961 chanzo kikuu cha maji kilikuwa Mto Ruvuma ambacho kililenga kutoa huduma ya maji kwa wakazi 3000 kwa mahitaji ya maji lita 400 kwa siku.
Beno aliongeza kuwa kuongezeka kwa wakazi wa huduma ya maji kutoka 5000 kwa mwaka 1961 hadi 236,936 sawa na asilimia 88% ya wakazi wote wa Songea ambao wanapata maji safi na salama.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa