MKUTANO wa mwisho ambao ulifanyika mwaka 1968 katika gogo hili, ndiyo uliosababisha kuongezeka kwa harakati za nchi ya Msumbiji kupata uhuru wake mwaka 1975.Gogo hili hivi sasa limewekwa katika eneo la Makumbusho ya Taifa ya Msumbiji.Katika gogo hili mwaka 1968 walikaa viongozi wa juu wa Msumbiji wakiwemo Rais wa Msumbiji hayati Samora Machel, Hayati Rais wa kwanza wa Tanzania Mwl.Julius Nyerere na viongozi wa juu wa chama cha FRELIMO wakifanya mkutano ambao uliikomboa nchi ya Msumbiji kutoka mikononi mwa ukoloni wa Kireno.Ukitembelea makumbusho haya ambayo yapo eneo la kihistoria la Matchedje nchini Msumbiji unapewa taarifa mbalimbali zikiwemo za kumbukumbu za kihistoria na kishujaa katika nchi ya Msumbiji kabla na baada ya uhuru.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa