Hali ya udumavu katika Mikoa ya kanda za nyanda za juu kusini ni wastani wa 42.9 ambapo alisema kiwango hicho kipo juu ya wastani wa Taifa ambao ni 31.8 licha ya kuwa na uzalishaji mzuri wa chakula na kuwa na ziada kubwa ya chakula.
Kauli hiyo imetolewa leo 08/08/2020 kwenye kilele cha maadhimisho ya maonesho ya Nanenane yaliyofanyika katika uwanja wa John Mwakangale Jijini Mbeya.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Mh. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassimu Majaliwa ambaye aliwakilishwa na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dr. Tulia Ackson .
Tulia alianza kwa kusema Mikoa ya kanda za nyanda za juu kusini inaendelea kuzalisha mazao mengi ya chakula ambapo kwa mwaka 2019-2020 uzalishaji wa chakula umekuwa tan Milioni 11,446,888.5 sawa na 91.4 kwa lengo la kuzalisha tan milioni 12,522,929.8 ambazo kwa sasa hutoshelevu wa chakula ni ziada kwa wastani 201.
Aliongeza kuwa kutokana na changamoto kubwa ya udumavu iliyojitokeza aliwaagiza viongozi wakuu wa Mikoa kukabiliana na hali hiyo ya udumavu pamoja na kufanya utafiti kujua sababu za kuwepo kwa viwango vya juu vya udumavu na kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.
Alibainisha kuwa kutokana na changamoto ya uhaba wa maeneo ya malisho ya mifugo ambapo hupelekea kutokea kwa migogoro kati ya Wakulima na Wafugaji kutokana na kuwa na idadi kubwa ya mifugo ikiwemo ng’ombe 3266000, mbuzi 1378237, na kondoo 343586, katika kupunguza migogoro hiyo Serikali imeanza kuboresha safu ya mifugo ili kuwa na idadi ya Mifugo inayoendana na ardhi tuliyonayo.
Alisema kuwa Serikali inaendelea kuweka mazingira mazuri ya usafirishaji kwa kuboresha miundombinu ya Barabara na uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe ili kuwezesha ndege za mizigo kutua usiku na mchana.
Aliongeza kuwa Serikali imeanza kuweka mkazo maalmu wa kuendeleza ushirika kutokana na baadhi ya wakulima kukata tamaa kwasababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika kutotekeleza wajibu wao. Hata hivyo alifafanua kuwa Serikali imeamua kuweka mkazo maalmu kwa mazao matano yaani chai, Kahawa, Korosho, Tumbaku na Pmba.
Kauli mbiu katika maadhimisho hayo ni: Kwa maendeleo ya Kilimo, Mifugo, na Uvuvi chagua viongozi bora 2020.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY,
KAIMU AFISA HABARI- MANISPAA YA SONGEA.
08/08/2020
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa