• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

HALMASHAURI Nyasa yamaliza kero ya wananchi kuliwa na mamba

Tarehe ya kuwekwa: September 8th, 2019

Wakazi wa Kata ya Kijiji cha Lundo, kata ya Lipingo wameupongeza uongozi wa Wilaya ya Nyasa, kwa kuwajengea daraja katika daraja la mto  Lwika.Daraja hilo linalounganisha, Kitongoji cha zambia na Kijiji cha Lundo  na kumaliza kero ya wakazi hao kuliwa na mamba.

Wakazi hao walitoa pongezi  wakati wa Ziara ya kamati ya Siasa, ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Nyasa, walipokuwa wanatembelea na kukagua miradi ya maendeleo, iliyotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa hivi karibuni katika Kata ya Lundo.

Wananchi hao walifafanua kuwa, kwa muda mrefu walikuwa wakishuhudia vifo vinavyotokana na kuliwa na mamba, waliokuwa wakikaa katika mto huo ,na kuwaua wakazi waliokuwa wakivuka kwa kuwa walikuwa wakilazimika kuingia katika mto huo ili  wavuke.

Waliongeza kuwa baada ya kukamilika kwa daraja  hakuna kifo chochote cha kuliwa na mamba kilichotokea katika kijiji hicho na wakazi wa kijiji hicho. Wamekuwa wakiishi kwa amani, bila hofu ya kuliwa na mamba  katika daraja hilo linalounganisha kitongoji cha Zambia na kijiji  cha Lundo.

Ofisa Mtendaji wa kata ya Lipingo, Kuno Ntini alithibitisha  daraja hilo ni Ukombozi katika kata yake kwa kuwa kumewafanya wanachi kutekeleza majukumu yao ipasavyo.  Awali walikuwa wakiwa na hofu ya kwenda shamba kwa hofu ya kuliwa na mamba katika daraja hilo lakini kwa sasa wanaendelea vizuri na  shughuli za maendeleo.

“daraja hili lilikuwa kikwazo sana kjatika shughuli za kimaendeleo, kwa kuwa watu walikuwa wakishindwa kufanya kazi kwa hofu ya kuliwa na mamba lakini tangu daraja likamilike hakuna kifo cha mamba kilichotokea”

Awali akisoma taarifa ya ujenzi wa daraja hilo, Kaimu meneja wa wakala barabara za mijini na vijijini (TARURA) wilayani hapa  Mageta Mteleke ,alisema serikali imetoa Shilingi milioni sabini na tisa nukta nne (79,400,000/=) mpaka kukamilika kwa mradi huu na inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya barabara ili kuharakisha maendeleo kwa wananchi.

Katubu wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilayani hapa Abasi Mkweta  kwa niaba ya chama hicho Wilayani hapa alipongeza juhudi zilizofanywa na Halmashauri ya kujenga daraja hilo na kuwaomba waendelee kutatua kero za wananchi kwa wakati ili kuwawezesha wananchi hao kupiga hatua za kimaendeleo kwa haraka.

“Napenda kuchukua fursa hii kukupongeza sana Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nyasa Bw.Jimson Mhagama kwa kutekeleza mradi huu ambao ulikuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo katika Kata hii wakazi walikuwa wakiliwa na mamba na hata wananchi wameufurahia sana mradi huu kwa kuwa tangu kukamilika kwake hakuna kifo cha mamba kilichojitokeza katika Daraja hilo” .

Aidha aliwaomba wananchi kutunza miundombinu ya daraja la mto Lwika ili iweze kudumu  na kusaidioa vizazi vijavyo.

NA NETHO CREDO NYASA  DC 0767417597

 

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa