HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma inaendelea kutekeleza miradi mikubwa kupitia fedha zilizotolewa na Serikali kwa kupitia programu ya uimarishaji na uendelezaji miji (ULGSP) kwa ajili ya kutekeleza miradi ya miundombinu.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Tina Sekambo ameitaja Miradi hiyo ni pamoja na machinjio ya kisasa, ujenzi wa kituo cha mabasi cha Mkoa na pia ujenzi wa barabara km 10.3 kiwango cha lami katika barabara za mitaa.
Amesema Kukamilika kwa miradi wa machinjio ya kisasa kutaboresha uchinjaji wa kisasa hivyo kuongeza ubora wa bidhaa za nyama na kwamba Pia kukamilika kwa barabara kwa kiwango cha lami katika manispaa hiyo kutaboresha mwonekano wa mji wa Songea.
"Kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha mabasi cha Mkoa kutaboresha sekta ya usafirishaji na kupunguza msongamano katikati ya mji hivyo kuruhusu kituo cha mabasi kinachotumika sasa kwa mabasi yaendayo wilayani na maeneo yanayo izunguka Manispaa ya Songea na hivyo kuongeza mapato'',amesisitiza Sekambo.
Hata hivyo amesema Halmashauri inaandaa mradi wa kimkakati ili kujenga soko la kisasa la Manzese ambalo litaboresha huduma kwa Wananchi na kuiletea mapato Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Pia Halmashauri imepima viwanja 150 eneo la kata ya Lilambo kwa ajili ya uwekezaji hususani kwenye sekta ya viwanda.
Imetolewa na
Victoria Ndejembi,
Kitengo TEHAMA Manispaa Songea,
22 Agosti 2018.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa