Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Ruvuma Victor Nyenza ambaye pia ni Mratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii iliyoboreshwa iCHF amesimamia zoezi la utoaji mafunzo kwa maafisa Waandikishaji 190 ambao wanatoka katika mitaa 95 iliyopo Manispaa ya Songea, iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya kata Mfaranyaki Manispaa ya Songea 02/09/2020.
Nyenza alisema kuwa Mkoa wa Ruvuma una Maafisa Waandikishaji 1354, kutoka katika Halmashauri 8 nane ambao pia watapata mafunzo haya ya Waandikishaji ambayo yataendelea kufanyika kwa nyakati tofauti ndani ya Mkoa wa Ruvuma kama ilivyoelekezwa kwenye Waraka namba (1) wa maboresho ya Mfuko wa Afya wa jamii wa mwaka 2018.
Lengo kuu la mafunzo haya ni kuboresha utendaji wa kazi wa Afisa Mwandikishaji pamoja na uboreshaji wa mchakato mzima wa usajili sahihi wa wanachama wa CHF ikiwa pamoja na ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mfumo wa Kieletroniki na kuacha kutumia mfumo wa kawaida wa malipo mkononi ambao ulikuwa unasababisha upotevu wa fedha za Serikali.
Aliongeza kuwa lengo kuu la Mkoa wa Ruvuma ni kufanya usajili kwa 50% ambapo hali halisi ya usajili Kimkoa ni 3.6%, Kwa Halmashauri ya Manispaa ya Songea ina lengo la kufanya usajili wa kaya 28820 sawa na 50% ambapo hali halisi ya usajili manispaa ya Songea ni 2.4% .
Alibainisha kuwa moja ya mkakati liyowekwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa Maafisa Waandikishaji wa mitaa/kijiji ndani ya Mkoa wa Ruvuma ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi bila ya upotevu wa mapato ya Serikali.
Alifafanua kuwa CHF iliyoboreshwa inanufaisha kaya yenye tegemezi 6 sita kama vile mkuu wa kaya, mwenza, na tegemezi wanne (4) wasiozidi miaka 18 kwa gharama ya shilingi elfu thelathini tu 30,000/= ambayo itatumika ndani ya mwaka mmoja.
IMETAYARISHWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
07.09.2020
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa