Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa nchini ambayo imebarikiwa kwa kuwa na neema ya vivutio lukuki na adimu vya utalii wa ikolojia na kiutamaduni.Hifadhi ya Gesimasowa yenye ukubwa wa kilometa za mraba zaidi ya 700 ambayo ipo katika Halmashauri ya Madaba Wilaya ya Songea,ni miongoni mwa vivutio adimu vya utalii.
Hifadhi hiyo ilianzishwa kama msitu wa hifadhi mwaka 1975 na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wa zamani Hayati Dk.Lawrence Gama mwaka 1975.Hatimaye mwaka 2015,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma katika kipindi hicho hayati Said Mwambungu alisimamia mchakato wa kupandisha hadhi msitu huo na kuwa hifadhi ya Taifa.
Kulingana na Challe,hifadhi ya Gesimasowa ni mapito ya ndege hao ambao wanatoka Kaskazini mwa Afrika kuelekea Afrika ya Kusini ambao wanafuata milima ya Livingstone iliyopo ziwa Nyasa na kwamba ndege hao pia wanapumzika Mwambao mwa ziwa Nyasa hasa katika eneo la Kihagara ambapo kuna mazingira ambayo yanavutia ndege hao kuishi.
Kwa mujibu wa Challe,Hifadhi ya Gesimasowa pia ina mfumo wa ikolojia wa pori la Selous kwa sababu ni mapitio ya wanyamapori wanaotoka katika Pori la Akiba la Selous wanapita kuelekea Bonde la ziwa Nyasa kupitia pori la Liparamba hadi Hifadhi ya Niasa nchini Msumbiji ambapo wanyama wanakwenda nchini Msumbiji na kurudi Tanzania.Wanyama ambao unaweza kuwaona katika hifadhi ya Gesimasoa ni tembo, simba,ndege, nyati, pofu na samaki adimu duniani aina ya mbelele na mbasa.
Mwandishi wa makala haya ni Albano Midelo
Mawasiliano yake ni albano.midelo@gmail.com,simu o784765917
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa