Chanzo cha mto Ruvuma kipo katika milima ya Matogoro iliyopo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.Mto Ruvuma ndiyo mto mrefu zaidi Afrika Mashariki wenye urefu wa kilometa 730.Unapofikia mpaka wa Tanzania na Msumbiji, takriban kilometa 200 baada ya chanzo, unageuka tena kuelekea mashariki hadi bahari ya Hindi kilometa 35.
Mto Ruvuma ukiwa kilometa 160 kabla ya kufika mdomoni bonde la Ruvuma unapanuka kuwa na upana wa kilometa 10, lalio la mto Ruvuma ni karibu mita 500 likiwa na visiwa vya mchanga. Wakati wa ukame katika Mto Ruvuma maji hupungu hadi watu kuvuka mto kwa miguu na wakati wa mvua umbali kati ya pande zote mbili unafikia zaidi ya kilomita moja.
Mdomo wa Mto Ruvuma uko Bahari ya Hindi kati ya Mtwara (Tanzania) na Rasi ya Delgado (Msumbiji). Mdomo wenyewe una umbo la delta. Athira ya maji kujaa au kupwa baharini huonekana kilometa 20 kabla ya mdomo wenyewe.Kabla kufika kwenye delta kuna feri inayobeba magari kati ya Tanzania na Msumbiji. Feri ilipelekwa hapa na mapadre Wabenedikto wanaofanya kazi pande zote mbili za mto.
albano.midelo@gmail.com
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa