HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imeanza kutoa huduma ya matatibu kwa wagonjwa mbalimbali kwa mfumo wa Hospitali Tembezi linalofanyika katika Hospitali Teule ya Wilaya Mtakatifu Gemma iliyopo Kata ya Miyuji Jijini humo.
Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma Dk. Hamad Nyembea amesema huduma ya Hospitali Tembezi ni jukwaa linalowakutanisha madaktari Bingwa wa fani mbalimbali za utabibu kama mgonjwa ya akina mama na watoto, Figo, Moyo, Koo na Pua, Kinywa na Meno, Shinikizo la Damu, Sukari, Tezi Dume, Shingo ya Kizazi, Macho, Masikio, pamoja na upasuaji wa mifupa na wa kawaida.
Huduma za matibabu kwa mfumo wa hospitali tembezi ulianza rasmi Juni 25 mwaka huu ambapo katika kipindi cha siku mbili wagonjwa 664 wamehudumia .Dk.Nyembea ametoa rai kwa wakazi wa Jiji la Dodoma na Wilaya za jirani hususan wanaosumbuliwa na maradhi mbalimbali kutumia fursa hiyo vizuri.Mfumo huu wa mataibabu endapo unatumika katika nchini nzima ikiwemo Manispaa ya Songea inaweza kusadia kuwafikia wagonjwa wengi ndani ya muda mfupi.
Habari hii ni kwa Hisani ya blog ya Manispaa ya Jiji la Dodoma.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa