Ni katika Kongamano lililofanyika Jana 25/02/2020 katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea
Mgeni Rasmi wa Kongamano la Tamasha ya Kumbukizi ya Vita vya MajiMaji ni Dr Willy Migodela Makamu Mkuu wa Chuo cha SOCAITE kilichopo manispaa ya Songea.
Dr Willy alizitaja Taasis au Wadau mbalimbali ambao wameshiriki katika kongamano hilo ni pamoja na Makumbusho ya Taifa, Wizara ya Maliasili, Idara ya Mali Kale, Ruaha National Park, Baraza la Makumbusho (M) Ruvuma, Wananchi Mbalimbali, Pamoja na baadhi ya wawakilishi wa wanafunzi kutoka Shule za Msingi na Sekondari zilizopo manispaa ya Songea.
Vita vya majimaji ni Vita vya Ukombozi vilivyopigana ili kunyofoa katika Utawala wa Kijerumani uliokuwa unaotesha mizizi yake nchini Tanzania, ili kupinga utawala wa kikoloni, kupinga kunyanyaswa, kunyang’anywa ardhi, kupinga uwepo wao katika himaya zao.
Aliitaja Mikoa ya Kusini Mashariki ya Tanzania ambayo Vita hivyo vilipigana katika Ardhi ya Mikoa ya Ruvuma,Njombe,Iringa,Morogoro,Lindi,Mtwara,Pwani,Dar es salaam, na Tanga(Pangani). Miongoni mwa makabila yaliyoshiriki katika kupigana Vita vya majimaji ni; Wangoni,Wasangu, Wahehe, Wamatumbi,Wamwera, Wangindo, Wapogoro, Wayao, Wandendeule,Wamatengo, Wabena, Wahehe na makabila mengine.
Kutokana na mapambano makubwa yaliyofanyika katika Kijiji cha Maposeni ambayo yalipelekea kukamatwa kiongozi Nkosi Mputa mnamo tarehe 10/01/1906 katika vijiji vya Peramiho, Kigonsera, Kingole,na Namabengo na Mjini Songea yalipelekea viongozi (100) wa kingoni kunyongwa 27/02/2020 ndio sababu ya kilele cha Tamasha la kumbukizi ya Vita vya Majimaji kufanyika kila mwaka.
KAULI MBIU “MCHANGO WA VITA VYA MAJIMAJI KATIKA KUENDELEZA NA KURITHISHA URITHI WA UTAMADUNI KWA MAENDELEO YA TAIFA”
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KAIMU AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa