• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

ILANI YA UTEKELEZAJI YATATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI SONGEA MJINI.

Tarehe ya kuwekwa: February 5th, 2023

Halmashauri ya Manispaa ya Songea Katika Kipindi cha mwezi Julai hadi Disemba 2022/2023 imepokea fedha jumla ya Tshs. 24,520,890,480.17 sawa na asilimia 52% ya fedha zilizotengwa shilingi  47,306,589,364 ambapo Kati ya fedha hizo, kiasi cha Tshs. 6,029,150,988.24 ni fedha za miradi ya maendeleo ambayo ni ujenzi wa madarasa 76 yenye thamani  ya Tshs. 1,520,000.00 na ujenzi wa hospitali ya wilaya awamu ya pili kwa kiasi cha shilingi 500,000,000.

Kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Halmashauri ya Manispaa ya Songea imekisia kukusanya kiasi cha shs 5,517,867,324.00 kutokana na vyanzo vya ndani vya mapato na hadi kufikia Disemba 2022 Halmashauri imekusanya kiasi cha shs 2,609,103,434.93 sawa na asilimia 47.2 ya lengo kwa mwaka ikiwa ni utekelezaji wa  Ibara 122(c) ambayo inatutaka  kuimarisha makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuimarisha makusanyo ya mapato katika vyanzo vilivyopo ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Hayo yamejili wakati wa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa CCM wa mwaka 2020 kuanzia Julai hadi Disemba 2022  iliyofanyika tarehe 04 Februari katika ukumbi wa Manispaa ya Songea ambayo yaliadhimishwa kuelekea kilele cha miaka 46  kuzaliwa kwa CCM tarehe 05/02 ambayo huadhimishwa kila mwaka.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya Songea Mjini Mwinyi Msolomi amewataka Viongozi mbalimbali kuacha Mipasuko ambayo itapelekea  kuzorotesha  shughuli za kimaendeleo.

Msolomi alisema lengo kuu la Serikali katika kuaajiri wataalamu ni kwa ajili ya kusimamia na kuratibu  shughuli shughuli zote za  Serikali pamoja na kusogeza huduma kwa wananchi,

Aliongeza kuwa katika kuelekea siku ya kilele cha maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCM Miaka 46 ambapo kilele cha  maadhimsho hayo yanafanyika Wilayani Tunduru, hata hivyo amewataka viongozi mbalimbali na wataalamu kuhakikisha wanapeleka wanafunzi waliochaguliwa kuijiunga   kidato cha kwanza shule.

Kwa upande wake katibu wa CCM Wilaya ya Songea Mjini James Mgego alianza kwa kutoa shukrani kwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa . Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Kusimamia na kuratibu  maendeleo  katika Sekta za miundombinu ya Barabara, madarasa, maji, umeme na Afya.

Mgego amewataka viongozi wa chama hicho ngazi ya Shina/ Tawi, Wilaya na Watendaji wa Serikali za Mitaa na Kata kuhakikisha wanatekeleza agizo lililotolewa kupitia kikao hicho la kufanya uhakiki wa wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao bado hawajaripoti shule.

Ilani hiyo imesomwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea ambaye aliwakilishwa na Mkurugenzi Manispaa ya Songea Dkt. Frederick Sagamiko ambaye alisema  Katika kutekeleza maelekezo ya Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 Halmashauri ya Songea ya Manispaa inatekeleza kazi mbalimbali za kiuchumi ambazo ni pamoja na Kilimo na biashara ambapo Kilimo huchangia asilimia 75 ya pato la Halmashauri ya Manispaa ya Songea ambapo jumla ya Hekari 29,745.61 zimetengwa  kwa ajili ya uwekezaji katika kata za Lilambo, Mwengemshindo, Tanga, Mletele na Ruhuwiko.

Dkt. Sagamiko alibainisha kuwa Katika kipindi cha Julai hadi Disemba 2022/2023 Jumla ya hekta 15,727.00 zimelimwa na matarajio ya mavuno ni tani 73,758.00 ambapo  Kwa msimu wa mwaka 2022/2023 malengo ni kulima hekta 25,522.30 na matarajio ya mavuno ni tani 117,933.50.

Katika mwaka fedha  wa fedha 2022/2023  Halmashauri imetenga 10% ya mapato ya ndani Kiasi cha Tshs 436,188,532.39 ambapo  hadi kufikia  mwezi Desemba 2022 jumla ya Tshs. 262,000,000.00  zimehamishwa kutoka akaunti ya makusanyo kwenda kwenye akaunti ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Alisema Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa  Halmashauri ya Manispaa ya Songea inahudumia mtandao wa Barabara jumla ya kilometa 513.75 kati ya hizo, kilometa 256.69 ni za Mjazio (Feeder Roads, 254.99  ni za Mkusanyo (Collector Roads) na Kilometa 2.07 ni za Jamii (Community Roads) Barabara kwa ujumla katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea imegawanyika katika makundi makuu manne ambapo jumla ya kilomita 49.50 ni barabara za Changarawe , Kilomita 33.01 ni barabara  za  lami , kilomita 430.49 ni barabara za udongo na Kilomita 0.55 ni barabara za mawe pia  kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Manispaa ya Songea imetengewa jumla ya TZS 2,571,280,000.00 kwa ajili ya  kufanyia matengenezo mtandao wake wa barabara.  “Dkt. Sagamiko,  alibainisha”

Aliongeza kuwa Katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Disemba 2022/2023  Halmashauri ya Manispaa ya Songea imepokea fedha kiasi cha Tshs. 750,000,000.00 kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa Hospitali ya Manispaa, Zahanati ya Makambi na ununuzi wa dawa, vifaa tiba na vitenganishi kwaajili ya vituo vya kutolea huduma za dawa. 

                                                                                                    

Naye Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano ametoa Rai kwa watendaji wa kata na mitaa  kushirikiana na wazazi kufanikisha kusimamia zoezi la wanafunzi wasioripoti shule na wale wote watakao kiuka taratibu hatua kali za kishria zitachukuliwa dhidi yao.

 

 

IMEANDALIWA NA;

AMINA  PILLY;

KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.








Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MKOANI RUVUMA

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma Awapongeza Wastaafu 86 wa Kada ya Ualimu Mkoani Ruvuma

    May 08, 2025
  • Kamati ya Siasa Wilaya Yaridhishwa na Hatua za Miradi ya Maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

YALIYOJIRI MAKABIDHIANO YA MBIO ZA MWENGE WA UHURU
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa