WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo ametoa wiki mbili kuanzia leo kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha wanabainisha maeneo ya ujenzi na mafundi watakaojenga madarasa 478 na mabweni 269.
Ameayasema hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa leo yanayofanyika katika ukumbi wa chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Jijini Dodoma.
Mhe. Jafo alisema kuwa tayari Serikali imetenga shilingi bilioni 29 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 478 mapya na Mabweni 269 ili kuhakikisha wananfunzi wote waliokosa nafasi ya kupangiwa kujiunga na kidato cha tano awamu ya kwanza wanapata katika uchaguzi wa awamu ya pili.
Mhe. Jafo amewataka Wakurugenzi hao kuhakikisha wanatumia muda mdogo kubainisha maeneo yatakayojengwa madarasa na mabweni kwa kutumia njia ya “Force Account” ili uchaguzi wa wanafunzi awamu ya pili uatakapofanyika na ujenzi huo uwe umekamilika.
Mhe. Jafo aliwaagiza Wakurugenzi hao kusimamia ujenzi huo na kuhakikisha unakamilika tarehe 30/08/2018 ili wanafunzi waliokosa nafasi ya kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya kwanza wanachaguliwa katika awamu ya pili na kutimiza ndoto za wanafunzi hao .
Mhe Jafo aliwaagiza Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha wanasimamia kwa weledi ujenzi wa miradi mbalimbali katika Halmashauri zao ikiwemo ya ujenzi wa madarasa na Mabweni ili kupunguza changamoto ya ukosefu wa madarasa nchini.
“Ninawaagiza Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Nchini kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ujenzi wa madarasa na mabweni kwa umakini wa hali ya juu ili dhamani ya fedha inayotolewa na Serikali iendane na majengo yatakayojengwa. Alisema Jafo
Aidha Mhe. Jafo alisema sambamba na ujenzi huo Serikali imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya vingine 98 na kuwataka kuhakikisha wanafanyakazi kwa weledi na umakini wa hali ya juu hasa katika suala zima la usimamizi wa miradi mbalimbali ili dhamani ya fedha zinazotolewa iendane na majengo yatakayojengwa.
Habari imeandikwa na Angela Msimbira OR-TAMISEMI
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa