• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

JAFO atoa maagizo mazito kwa waganga wa Wilaya na Mikoa nchini

Tarehe ya kuwekwa: August 16th, 2018

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya  kusimamia ujenzi wa vituo vya afya unaoendelea kote nchini pamoja na kuweka udhibiti imara wa upotevu wa fedha ili kusiwe na upungufu wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma nchini.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri zote nchini uliofanyika katika ukumbi wa LAPF leo Jijini Dodoma.

“Fanyeni kazi kwa weledi kwani msipotimiza wajibu wenu ipasavyo tutadumaza afya za wananchi, natamani itakapofika mwaka 2020 kila mwananchi azungumze faraja kwenye sekta ya afya”, alisema Waziri Jafo.

Aidha,Waziri huyo alisema katika ukusanyaji wa mapato hauridhishi,  hivyo kufanya vituo vingi kuwa na makusanyo madogo ya mapato ya kila siku licha ya kuwahudumia wananchi wengi.

Kwa upande wa kuboresha huduma za afya nchini, Waziri Jafo alisema wakati Serikali ya Awamu ya Tano inaingia madarakani kulikuwa na vituo vya afya 115 vilivyokuwa  na uwezo wa kufanya upasuaji wa dharura. Kwa sasa vipo vituo 210 ambavyo vinatoa huduma hiyo , sawa na asilimia 95

Aliendelea kufafanua kuwa katika bajeti ya Mwaka wa Fedha 2018/2019 Serikali imetenga takribani bilioni 105 ambapo ajenda kubwa ni ujenzi wa Hospitali za Wilaya 67 hivyo kufanya vituo 307 vitakavyokuwa vinafanya upasuaji wa dharuara.

Waziri Jafo alisema kuwa uwepo wa vituo hivyo kutapunguza vifo vya akina mama wajawazito wakati wa kujifungua na kupunguza changamoto za utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.

Aliwapongeza Waganga Wakuu wa Mikoa na wa Wilaya kwa kuisaidia Serikali  kuokoa fedha katika ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya afya kwa kutumia taaluma zao ambazo zimesaidia kujenga vituo bora kulingana na mahitaji.

Amewaagiza washiriki hao kuhakikisha wanaongeza kasi katika suala zima la ukusanyaji wa mapato katika Hospitali za Mikoa na Wilaya kwa kuhakikisha wanafunga mifumo ya kielektoroniki ya ukusanyaji wa mapato.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Afya), Mhe. Zainabu Chaula alisema ili kupunguza changamoto za afya nchini inabidi kufanyakazi kwa weledi, ushirikiano katika ngazi zote za uongozi, pamoja na wadau wa sekta ya afya nchini.

Amesema kuwa uwajibikaji wa pamoja na utumishi wenye weledi katika utoaji wa huduma za afya ndio msingi wa uboreshaji wa mazingira ya kutolea huduma za afya kuelekea Tanzania ya Viwanda na uchumi wa kati

Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi. Mussa Iyombe amewaagiza watumishi wa Sekta ya afya  kutoka OR-TAMISEMI na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia  , Wazee na watoto kufanya kazi kwa weledi ili kuweza kutatua changamoto za afya kwa wananchi maskini wanaohitaji huduma katika jamii.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya alihimiza umuhimu wa matumizi ya takwimu sahihi katika upangaji wa bajeti na mipango mingine ya sekta ya afya hususani kwenye vifo vitokanavyo na akina mama wajawazito na watoto wachanga kwani hivi sasa kila mwaka akina mama wajawazito wapatao elfu kumi na moja hufariki.

Anaandika Angella Msimbira- OR TAMISEMI

Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • RC Ruvuma Awapongeza Wastaafu 86 wa Kada ya Ualimu Mkoani Ruvuma

    May 08, 2025
  • Kamati ya Siasa Wilaya Yaridhishwa na Hatua za Miradi ya Maendeleo

    May 06, 2025
  • Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Apongeza kwa Utekelezaji wa Miradi

    May 05, 2025
  • Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Awataka Waajiri kuzingatia Misingi ya Utawala Bora

    May 01, 2025
  • Tazama zote

Video

Mkuu wa Wilaya ya Songea Akizindua Stendi ya Bajaji - Songea
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa