Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, amewapongeza walimu wastaafu kwa kulitumikia Taifa kwa uzalendo, uaminifu na weledi mkubwa katika kipindi chao cha utumishi.
Akizungumza katika hafla ya kuwaaga walimu hao iliyofanyika katika ukumbi wa Anglikana, Kanali Ahmed alisema kazi ya ualimu ni ya kipekee, yenye uvumilivu na moyo wa kujitoa.
“ kazi ya uwalimu ni kazi ya wito, ni sadaka na ni huduma kwa vizazi visivyo na idadi lakini mmevumilia mazingira magumu ya kipato mmeendelea kulitumikia Taifa kwa bidii na uaminifu mkubwa” alisema Kanali Ahmed.
Aidha amewataka walimu wastaafu kuendelea kushiriki katika ujenzi wa jamii, kwa kuwa uzoefu wao bado unahitajika katika maendeleo ya elimu.
Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Ruvuma, Edith Mpinzile amesema idadi ya walioangwa ni walimu 86 ambao wamestaafu kuanzia Januari 01, adi Desember 31, 2024.
Mpinzile, ameongeza kwa kusema ameandaa tukio hilo kwaajili ya kutambua thamani na mchango wa walimu katika jamii. Huku akieleza jambo hili ni mpango wa mkoa na litakuwa linafanyika kila mwaka.
Mwenyekiti wa Walimu Wakuu Mkoa wa Ruvuma, Mwl Siwema Ahmed amewashauri wastaafu kuacha kufanya biashara wasizowahi kuzifanya na wasimamie yale waliyokuwa wakiyafanya wakati wa utumishi wao.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa