MACHI nane mwaka huu ni siku ya maadhimisho ya siku wanawake Duniani,Maadhimisho hayo katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma yamefanyika eneo la Namanditi Kata ya Ruhuwiko ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Songea Jaji Sekela Moshi ambaye pamoja na mambo mengine amezungumzia changamoto ya sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ambayo katika kifungu cha 13 inabainisha kuwa mtoto wa kike anaweza kuolewa akiwa na miaka 15.
Kulingana na sheria hiyo mtoto wa kiume anaruhusiwa kuoa akiwa na umri wa miaka 18 na kwamba kifungu hicho hicho kinaeleza kuwa mtoto wa kike anaweza kuolewa akiwa na umri wa miaka 14 kwa ruhusa ya mahakama ambapo katika kifungu cha 17 kinaeleza kuwa ndoa ya binti inaweza kupangwa na wazazi pasipo kupata ridhaa ya mtoto wa kike,
Hata hivyo amesema sheria ya kanuni ya adhabu ,sura ya 16,kifungu 138 inaruhusu mtoto wa kike kuolewa katika umri wa miaka 12 kwa masharti kuwa hawatakaa kinyumba mpaka atakapotimiza miaka 15 na kwamba sheria zote zinakinzana kabisa na sheria ya mtoto ambapo ameshauri sheria zote zinapaswa kurekebishwa ili ziendane na sheria ya mtoto ambayo inatafsiri kuwa mtu yeyote mwenye umri wa chini ya miaka 18 anatambulika kuwa mtoto.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa