Kwa kuzingatia kifungu cha 89A cha sheria ya Taifa ya uchaguzi sura 343 na kifungu cha 88A cha sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Sura 292, Tume haitasita kumchukulia hatua Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo/ Kata ambaye atasababisha makosa ya uchaguzi kwa maksudi atachukuliwa hatua za kisheria.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi (NEC) Dr. Wilson Charles akiwa katika kikao na Wasimamizi wa Uchaguzi Jimbo cha kanda kilichojumuisha mikoa sita yaani Mkoa wa Ruvuma, Mbeya, Njombe, Iringa, Lindi, na Mtwara kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea leo 17.10.2020.
Dr. Wilson alisema “ lengo kuu muhimu la kikao hicho ni kukumbushana masuala muhimu ya yatakayosaidia kuendesha vizuri zoezi la uchaguzi Mkuu ambao unatarajia kufanyika tarehe 28 oktoba mwaka huu kama ambavyo ilivyokuwa ikifanyika katika mazoezi mengine yanayopelekea kukutana pamoja. Aliongeza kuwa mkutano huo umeandaliwa kwa kanda sita ili kuwapunguzia umbali wa kusafiri kutoka kwenye maeneo yao na kuokoa muda katika kipindi hiki cha maandalizi ya Uchaguzi.
Alisema matarajio ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni kuwa na wasimamizi ambao watakuwa wameelewa vizuri maelekezo yote yaliyotolewa na Tume na kuweza kufanikisha kusimamia zoezi la uchaguzi wa udiwani, Ubunge, na Rais.
Alibainisha kuwa baada ya kukamilika zoezi la uandikishaji daftari la wapiga kura lenye jumla ya wapiga kura 29,188,347 na kwa upande wa Zanzibar jumla ya wapiga 566,352 wameandikishwa. Pia katika uchaguzi mkuu mwaka huu kutakuwa na jumla ya vituo 81,568 ikiwa Tanzania bara kutakuwa na jumla ya vituo 80,155 na Tanzania Visiwani jumla ya vituo 1413.
Alisema ongezeko hilo ukilinganisha na mwaka 2015 kulikuwa na jumla ya wapiga kura 23,166,144 na kufanya kuwa na ongezeko 6,000,000 la wapiga kura. Alifafanua kuwa kila kituo kitakuwa na wapiga kura wasiozidi 450-500, pia akinamama wajawazito, wenye watoto wadogo, wazee, na walemavu watapewa kipaumbele.
Aidha, kutakuwepo na vituo vya wazi kwa kuzingatia maelekezo ya Tume pia ujenzi wa vituo kwa kuzingatia idadi ya mawakala pamoja na kuweka eneo la kitutuli ili mpiga kura aweze kupiga kura kwa uhuru na kwa haki.
Alisisitiza kutumia majengo ya umma kama shule, zahanati, na ofisi za kata ili kutunzia vifaa vya uchaguzi na kuhakikisha uwepo wa usalama wa vifaa pamoja na ulinzi wa eneo husika. Alisisitiza.
Dr. Wilson aliwaasa wasimamizi wa Uchaguzi kubandika mabango ya mshale makubwa na madogo ili mpiga kura aweze kuona kituo kirahisi.
Alisema vituo vyote vinatakiwa kufunguliwa saa moja kamili 1:00 asubuhi bila kusahau sheria ya uchaguzi inakutaka ukishapiga kura unatakiwa kuondoka kituoni.
IMETAYARISHWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa